Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Mlezi wa Mkoa wa Tanga Ndugu HEMED SULEIMAN ABDULLA amewataka wana CCM wa Mkoa wa Tanga kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa inaotarajiwa kufanyika mwenzi November 2024.
Ameyasema hayo wakati akipokea tarifa ya Chama na Serikali mara baada ya kuwasili Mkoani humo katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga Mhe. Hemed amesema ushindi kwa Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu ujao ni lazima kuanzia ngazi ya Mitaa ,Vijiji hadi Vitongoji kwa pande zote mbili za Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Mjumbe huyo ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Amesema akiwa Mlezi wa Mkoa wa Tanga atahakikisha kuwa ndani ya Mkoa huo CCM inashinda nafasi zote za uongozi zitakazogombaniwa kama ibara ya Tano ( 5) ya katiba ya ccm inavyosema kuwa ushindi lazima.
Sambamba na hayo malezi wa chama hicho Mkoa wa Tanga amewataka viongozi wa CCM kuhakikisha wanadumisha umoja, mshikamano na Upendo uliopo baina yao katika kukitumikia chama na Serikali ili kuhakikisha wanawasaidia viongozi wakuu wanchi kuwaletea maendeleo wananchi wake wakiwemo wana CCM.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. BATILDA BURIAN amesema Mkoa wa Tanga unaendelea kuitekeleza vyema Ilani ya CCM kwa kuekeza katika Miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya maji safi na salama ambapo changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa maji ndani ya Tanga imeondoka pamoja na zoezi la kusambaza nishati ya umeme atika vijiji vyote 779 limekamilika na kwa sasa wanajipanga kuvifikia vitongoji vyote ndani ya mkoa wa Tanga ili ifikapo 2025 kazi hio imekamilika kwa mafanikio.
Dkt. BATILDA amesema Sekta ya Elimu katika Mkoa wa Tanga imezidi kuimarika kuanzi shule za msingi hadi sekondari , ujenzi wa nyumba za walimu na mabweni ya wanafunzi pamoja ujenzi wa vyuo vya Veta unaendelea katika Wilaya zote za Tanga sambamba na kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato katika Mkoa huo.
Mapema akisoma taarifa ya Chama Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Ndugu SULEIMAN SANKWA amesema CCM Mkoa wa Tanga imejipanga kusajili wanachama wapya zaidi ya laki moja hadi ifikapo Disemba 2024 ambapo zoezi hilo linaendelea vizuri.
SANKWA amesema Mkoa wa Tanga umedhamiria kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2025 na kumuhakikishia Mlezi wao kuwa Tanga itaendelea kufanya vizuri katika nyanja ya Siasa na Uchumi.
Imetolewa na kitengo cha Habari ( OMPR)
LEO tarehe 16.08.2024