Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema katika utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020 hadi 2025 , Serikali imedhamiria kusimamia ubora wa bidhaa kwa kuziweshesha taasisi zinazosimamia ubora ikiwemo Taasisi ya viwango Zanzibar (ZBS) kwa kuwa na maabara za kisasa na wataalamu wenye uwezo kwa kazi upimaji na ukaguzi.
Dkt.Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 6 Agosti 2024, alipofungua kituo cha ukaguzi wa vyombo vya moto, Maruhubi Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua ya kuimarisha miundombinu ya ZBS kwa kujenga kituo cha ukaguzi wa vyombo vya moto ambacho amekifungua.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itaendelea kufanya juhudi na kuchukua hatua za kuhakikisha wananchi wanakuwa salama kwa kujenga miundombinu imara kuwezesha shughuli za kusimamia ubora ziwe za kisasa kwa kuwapatia majengo ya maabara , vifaa vya kisasa na wataalamu.