Home » » DKT. NCHEMBA ATETA NA SAUDI FUND FOR DEVELOPMENT

DKT. NCHEMBA ATETA NA SAUDI FUND FOR DEVELOPMENT

Written By CCMdijitali on Friday, December 20, 2024 | December 20, 2024

 Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameongoza ujumbe wa Mawaziri wenzake akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe., Dkt. Selemani Jafo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, kutembelea Mfuko wa Maendeleo wa Saudi Arabia (Saudi Fund for Development-SFD), Mjini Riyadh nchini Saudi Arabia, ambapo walizungumza na Mwenyeji wao, Mkurugenzi Mtendaji wa Saudi Fund, Bw. Sultan Al-Marshad, na kujadili kwa kina masuala ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Mfuko huo na Tanzania.


Mhe. Dkt. Nchemba, aliishukuru Saudi Arabia kupitia Mfuko huo kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika sekta za maji, afya, nishati na ujenzi wa miundombinu ya barabara, ikiwemo ukarabati wa Mradi wa Maji mkoani Mara (USD 15m), Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe (USD 25m), ujenzi wa Barabara za Vijijini Awamu ya Pili-Zanzibar (USD 11.4m), Ukarabati na Upanuzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja-Zanzibar (USD 15m) na kushirikiana na wadu wengine kufadhili Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Umeme wa msongo wa 220kV kuanzia Benako mkoani Kagera hadi Kyaka (USD 105.4m). 


Mazungumzo hayo pia yalishuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Moh’d Juma Abdalla, Mkuu wa Idara Mashariki na Kati Mhe. Balozi Abdalah Abasi Kilima, Kamishna wa Idara ya Madeni-Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine na Kaimu Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Robert Mtengule.













Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link