Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameisisitiza jamii kuwaanda Watoto na Vijana kwa Elimu ya Dini ya mapema ili kuwajenga kuwa raia bora wa baadae.
Alhaj Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 13 Disemba 2024, alipofungua Zawiya ISHAAT AUSWAF NNABIYY iliopo Pitanazako Mbalungini ,Wilaya ya Kaskazin B, Unguja.
Amefahamisha kuwa kuwapatia Elimu ya mapema Vijana kunatengeneza Taifa Bora na hofu ya Mwenyezi Mungu.
Alhaj Dk. Mwinyi amewapongeza Waumini wa dini ya Kiislamu wa Eneo hilo kwa kujenga Jengo zuri la Zawia.
Akizungumzia suala la Amani Alhaj Dk. Mwinyi amewasisitiza Viongozi wa dini na Wanasiasa kutumia Majukwaa yao Kuhubiri Amani wakati nchi ikielekea katika Uchaguzi Mkuu 2025.
Vilevile Alhaj Dk. Mwinyi amewanasihi Waumini kuendelea kuiombea nchi Amani, Mshikamano ,Upendo na Umoja.
Ufunguzi huo wa Zawia umeambatana na Dua maalum ya Kumuombea Rais Dk. Mwinyi na Taifa kwa Ujumla na hatimae Alhaj Dk. Mwinyi alijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu kwa Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Mbalungini uliopo Pembezoni mwa Jengo la Zawia.