Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amewataka makandarasi wanaopatiwa kandarasi za ujenzi wa barabara za TARURA kutekeza miradi hiyo kwa ufanisi na kwa wakati kama ilivyo makubaliano ya katana.
Katimba ametoa maelekezo yake wakati wa ziara yake ya kikazi katika jiji la Dar Es Saalam ya kukagua barabara za TARURA katika jiji hilo kwa majimbo ya Ukonga na Segerea na kuona maeneo zitakapojengwa barabara mpya na barabara zitakazoboreshwa katika mradi wa awamu ya pili ya uendelezaji wa Halmashauri ya jiji la Dar Es Salaam (DMDP II) katika majimbo hayo.
“Wakandarasi wanapopewa Kazi hizi iwanajukumu la msingi Ła kuhakikisha wanatimiza jukumu lao kimkataba wahakikishe barabara hizi wanazijenga kwa mujibu wa mkataba ndani ya muda kusiwe kuna kusuasua kwasababu wananchi wanataka kuona tija kubwa ambayo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamilia iweze kufika kwao ya kuwajengea Miundombinu mizuri ya barabara” amesema.
Akisistiza hili Mhe. Katimba ameendelea kusisitiza kuwa barabara hizo zinazojengwa zinasaidia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa nchi vilevile kuwasaidia wananchi kufikia huduma za msingi za kijamii.
Kwa Upande wake mbunge wa jimbo la Segerea Mhe. Bonah Kamori ameiomba serikali kupitia Ofisi ya Rais - TAMISEMI kuwahimiza wakandarasi wasichelewe ili barabara hizo zijengwe na wananchi waendelee na shughuli za kiuchumi na kufikia huduma za msingi hasa katika kipindi cha mvua.
Naibu Waziri Mhe. Katimba ametmbelea barabara za Pugu-Majohe-Viwege kilomita 10.5, Banana-Kitunda-Kivule-Msongo kilomita 12.6 za jimbo la Ukonga na Bonyokwa-Zahanati kilimita 1.46, Bonyokwa mwisho kilomita 3.2, Segerea Kusini kata ya Segerea kilomita 0.69 za jimbo la Segerea.