Home » » MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- AKABIDHI VIFAA VYA UJENZI KWA VIONGOZI WA UVCCM

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- AKABIDHI VIFAA VYA UJENZI KWA VIONGOZI WA UVCCM

Written By CCMdijitali on Sunday, January 26, 2025 | January 26, 2025

 MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- AKABIDHI VIFAA VYA UJENZI KWA VIONGOZI WA UVCCM- TUNGUU - MKOA WA KUSINI -UNGUJA


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amewataka Viongozi wa CCM, wanachama na wapenda maendeleo kujitolea katika kuchangia na kuunga mkono ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo inayojengwa na chama pamoja na  Serikali kwa maslahi ya Taifa. 

Ameyasema hayo wakati alipofanya  ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo cha Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi ( UVCCM ) kinachojengwa Tunguu  Mkoa wa Kusini Unguja na kuchangia vifaa mbali mbali ili kuendeleza ujenzi huo. 

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amekabidhi saruji mifuko elf moja(1000), gari kumi (10) za mchanga na shilingi milioni tano (5) zitakazosaidia katika kuwapatia huduma vijana na CCM wanaojitolea katika ujenzi wa chuo hicho na kazi nyengine za Jumuiya ya UVCCM. 

Mjumbe huyo wa kamati kuu ya halmashauri kuu amesema Chama cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla wanatambua  kuwa nguvu na mchango wa vijana wa UVCCM katika kukijenga na kukiimarisha Chama hasa katika kusimamia ujenzi wa chuo cha UVCCM kitakachowafaundisha vijana kuwa watiifu na wazalendo kwa Taifa lao pamoja na kuwafundisha namna ya kujitegemea kiuchumi. 

Mhe. Hemed amesema kuwa changamoto zinazowakabili UVCCM hasa katika ujenzi wa chuo hicho Serikali itazifanyia kazi  ili kuweza kufanikisha malengo ya ujenzi huo kwa maslahi ya  chama cha mapinduzi na kuiwezesha jumuiya ya Umoja wa vijana kupiga hatua kimaendeleo. 

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesemea kuwa amefarajika kuona kazi kubwa inayofanywa na vijana wa umoja wa vijana wa CCM ya kujitolea katika kukiendelezaa na kukijenga chama ambapo ameahidi kuwa chama kitakuwaa bega kwa bega na vijana hao. 

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka vijana kuendelea kuitunza amani iliyopo nchini hasa katika kupindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na kuwaahidi kuwa watahakikisha chuo hicho kinamalizika katika viwango, ubora na hadhi ya  hali ya juu kwa maslahi mapana ya Vijana wa CCM na Taifa kwa ujumla. 

Nae Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mohamed Ali Mohamed ( KAWAIDA ) amesema dhamira ya ujenzi wa Chuo hicho ni kuendelea  kutengeneza makada wa CCM na viongozi wenye uchungu na  uzalendo wa nchi yao pamoja na kuwafunza namna bora ya kujiendeleza kiuchumia katika harakati zao za maisha. 

Kawaida amemshukuru Mhe.Hemedi kwa maamuzi yake ya kutembelea ujenzi wa chuo hicho pamoja na mchango wake alioutoa katika kuendeleza ujenzi huo na kuahidi kuwa atahakikisha vijana wa CCM wanakuwa wamoja, watiifu na wenye utayari wa kukipambani chama ili kizidi kutekeleza Ilani kwa vitendo. 

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM anaefanyia kazi zake Zanzibar Ndugu ABDI MAHMOUD ABDI amesema kumalizika kwa ujenzi wa chuo cha UVCCM utawanufaisha zaidi ya vijana elfu  4 ambao watapatiwa mafunzo mbali mbali chuoni hapo yakiwemo ya uzalendo kwa chama na Taifa lao pamoja stadi za maisha. 

Amesema ujenzi huo utajumuisha mabweni mawili ya wanawake na wanaume, kumbi za mikutani, chumba cha wageni mashuhuri, Madarasa, zahanati pamoja na viwanja vya michezo mbali mbali ambapo mkandarasi na wajenzi wa chuo hicho ni vijana kutoka UVCCM. 

Abdi amesema UVCCM wanaishukuru Serikali kwa kuendelea kuwapa kipaombele vijana na kuomba kusaidiwa kutatuliwa changamoto zao zinazowakabili ikiweno ya kuvamiwa  kwa eneo lao lililopa Tunguu ambalo limetengwa maalum kwa ajili ya shuhuli za UVCCM. 

 

Imetolewa na Kitengo cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe..26 / 01 / 2025



Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla akikabidhi vifaa mbali mbali vya Ujenzi kwa Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Cha UVCCM kinachojengwa Tunguuu Mkoa wa Kusini Unguja .


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link