Home » » WAZIRI KOMBO AONGOZA UJUMBE WA WIZARA

WAZIRI KOMBO AONGOZA UJUMBE WA WIZARA

Written By CCMdijitali on Wednesday, January 22, 2025 | January 22, 2025

WAZIRI KOMBO AONGOZA UJUMBE WA WIZARA KWENYE MKUTANO NA KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA KATIBA NA SHERIA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameongoza ujumbe wa Wizara kwenye mkutano na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria uliofanyika tarehe 21 Januari 2025 jijini Dodoma.


Mkutano huo pamoja na masuala mengine ulilenga kujadili Muswada kuhusu mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, ikiwemo mabadiliko ya Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 na Sheria ya Ardhi Sura 113 kama hatua muhimu ya kuwezesha utekelezaji wa hadhi maalumu kwa raia wa nchi nyingine wenye asili ya Tanzania.


Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje umejumuisha Viongozi wa Wizara wakiwemo Naibu Mawaziri Mhe. Cosato Chumi (Mb.) na Mhe. Dennis Londo (Mb.) anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki, Katibu Mkuu Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Naibu Katibu Mkuu Balozi Said Shaib Mussa na Watumishi wengine.









Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link