Home » » RAIS MWINYI: SMZ ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWENYE BIMA.

RAIS MWINYI: SMZ ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWENYE BIMA.

Written By CCMdijitali on Thursday, February 20, 2025 | February 20, 2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Kushirikiana  na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Itaendelea kuweka Mazingira  Wezeshi kwenye soko la Bima ili kuongeza Pato la Taifa kupitia Sekta hiyo.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipopokea  Taarifa ya Soko la Bima kwa Mwaka 2023  iliofanyika  Hoteli ya Verde , Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi. 

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Zina dhamira ya dhati ya kuleta Maendeleo kwa Wananchi kutokana na Mageuzi makubwa yanayoendelea  kufanyika katika sekta zote za Kiuchumi.

Amefahamisha kuwa ili Mageuzi hayo yafanikiwe ni vema Sekta ya Bima iendane na Kasi ya Serikali zote mbili kwa kujikita kwenye Ubunifu na Matumizi ya Teknolojia na Watoa Huduma za Bima na Wadau wote wafanye kazi kwa Weledi na Ushirikiano.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amesisitiza kuongezwa jitihada zaidi katika Matumizi ya Tehama, Ubunifu wa bidhaa za Bima na utoaji wa Elimu ya Bima kwa Wananchi.

Vilevile  Rais Dkt.Mwinyi amebainisha kufanyika kwa Utafiti wa aina ya Vihatarishi vinavyotakiwa kupewa kinga  kupitia Bima kwa Mali za Serikali na Mamlaka ya Bima   Ipitie Sheria na Kanuni mbalimbali za Bima ili ziendane na Mazingira  ya sasa na Ukuaji wa Uchumi.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amewasisitiza Wananchi na Wadau kuendelea kutumia huduma za Bima  na Mamlaka husika zifanye bidii ya kuhakikisha  Nchi inanufaika na Huduma hizo.

Ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania kwa Kuanzisha Ofisi ya TIRA kanda ya Unguja na Ofisi ya Kanda ya Pemba na kusisitiza Kutolewa Elimu zaidi kwa Wananchi ili wapate Uelewa zaidi wa Masuala ya Bima.



















Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link