Home » » RAIS MWINYI: TUSIPANDISHE BEI ZA BIDHAA ZA VYAKULA WAKATI WA RAMADHANI

RAIS MWINYI: TUSIPANDISHE BEI ZA BIDHAA ZA VYAKULA WAKATI WA RAMADHANI

Written By CCMdijitali on Monday, February 24, 2025 | February 24, 2025

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuridhishwa na upatikanaji wa Bidhaa za Vyakula na kuwataka Wafanyabiashara Kutopandisha Bei wakati Ramadhani itakapoanza.


Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipotembelea Masoko ya Jumbi , Mwanakwerekwe na Darajani kuangalia Mwenendo wa Biashara na Upatikanaji wa Bidhaa za Vyakula kuelekea Mwezi Wa Ramadhani.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inajipanga kwa ajili ya Ujenzi wa Masoko mengine maeneo mbalimbali ili kila Mfanyabiashara afanye biashara kwenye mazingira rasmi .

Kuhusu Suala la Usafi wa Masoko ameuagiza Uongozi wa Masoko hayo kutafuta njia Bora zaidi ya Uhifadhi wa Bidhaa za Wafanyabiashara ili Masoko kuwa safi wakati Wote.

Amezielekeza Taasisi zinazosimamia Masoko hayo kuhakikisha Upatikanaji wa Huduma ya Maji na Vipooza hewa katika Masoko yote pamoja na kuimarisha Usafi.

Ziara hiyo ya Rais Dkt, Mwinyi ni ya Kwanza tangu kufunguliwa kwa Masoko Mapya ya Jumbi , Mwanakwerekwe na Ukarabati Mkubwa wa Soko la Darajani.










Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link