Home » , » UCHAGUZI MKUU UTAFANYIKA, WANA-CCM, WANANCHI JIANDAENI - WASIRA

UCHAGUZI MKUU UTAFANYIKA, WANA-CCM, WANANCHI JIANDAENI - WASIRA

Written By CCMdijitali on Tuesday, February 11, 2025 | February 11, 2025



Na Mwandishi wetu, Mwanza

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uchaguzi mkuu wa mwaka huu utafanyika kama ulivyopangwa kwa taratibu za kisheria, na kwamba hakuna chombo cha serikali wala chama cha siasa chenye mamlaka ya kuuahirisha.


Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira, leo Februari 11, 2025 alipohutubia mkutano mkutano katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Wasira amesema watu wanaotoa hoja kwamba uchaguzi mkuu hautafanyika hadi yawepo mabadiliko ya Katiba wanajisumbua kwa kuwa makubaliano yalishafanyika kuwa mabadiliko ya Katiba yatafanyika baada ya uchaguzi mkuu, hivyo hakuna anayeweza kuahirisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu kwa namna yoyote.

“Tumekubaliana tumalize uchaguzi, zile sheria za uchaguzi zifanyiwe marekebisho, wabunge wanajua Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani imepitishwa na Bunge, Sheria ya Vyama vya Siasa imefanyiwa marekebisho na imepitishwa na Bunge.


“Chadema wamekuwa na msemo wao maarufu ‘no reform no election’ (kama hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi), sasa mimi hapa nasema leo uchaguzi mkuu utafanyika. Wanaosema uchaguzi hautafanyika mpaka mabadiliko yafanyike wanajisumbua, uchaguzi utafanya na Watanzania wajiandae.


“Sisi ni Chama cha siasa lazima tufanye uchaguzi ili tuendelee kuleta maendeleo ya Watanzania. Tumewaambia hakuna tunachoogopa kwa sababu hata Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 wameshindwa kuweka wagombea. Halafu wakishindwa wanasingizia CCM,” amesema Wasira.


Amesisitiza kuwa kwa taratibu za kisheria, si chombo cha serikali wala chama cha siasa kina uwezo wa kuahirisha uchaguzi mkuu, huku akifafanua kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kisheria inalo jukumu la kutangaza tarehe ya uchaguzi, lakini haina uwezo wa kuahirisha.

“Na kama kutakuwa sababu ya uchaguzi mkuu kusogezwa mbele au kuahirishwa basi ni kwa sababu ya uwepo wa vita lakini kwa bahati nzuri nchi yetu haina vita, iko salama na kazi ya kuleta maendeleo inaendelea. Hivyo hakuna chama cha siasa kinaweza kuahirisha uchaguzi na suala la mabadiliko ya Katiba ni la kisheria.


#KaziIendelee

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link