Home » , » MAWAKALA SEKTA YA MIILKI WATAKIWA KUJISAJILI

MAWAKALA SEKTA YA MIILKI WATAKIWA KUJISAJILI

Written By CCMdijitali on Wednesday, February 12, 2025 | February 12, 2025

 Na Munir Shemweta, WANMM ARUSHA

 

Mawakala wa Milki nchini wametakiwa kujisajili katika mfumo wa Wizara ya Ardhi ili kuingia kwenye mfumo rasmi utakaowezesha kutambulika.

 

Hayo yameelezwa leo tarehe 12 Februari 2025 na Mratibu wa Mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa Wadau wa Sekta ya Milki Bi. Nuru Kimbe, mjadala uliofanyika mkoani Arusha.

 

Amesema, ni vizuri mawakala wa milki wakajisajili katika mfumo ili waweze kutambulika katika kipindi hiki ambacho wizara inategemea kuwa na sheria ya milki.

 

"Nasisitiza mawakala waweze kujisajili na waweke ‘details’ za masingi kama anuani na mahali wanapofanyia kazi". Amesema Bi. Nuru

 

Kwa mujibu wa Bi. Kimbe ambaye ni Afisa kutoka Kitengo cha Milki Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, faida za kujisajili ni pamoja na kutambulika na serikali kitu alichokieleza kitarahisisha kazi kwa mawakala ambapo amesema hatua hiyo itarahisisha katika kazi zao kama wakala na kuwafikia wateja sambamba na kuaminika zaidi.

 

Amebainisha kuwa, kwa sasa mijadala inafanyika kwenye majiji ambako soko la milki linafanyika sana na kuitaja majiji hayo kuwa ni Dar es Salaam, Dodoma, Arusha na Mwanza.

 

Hata hivyo, amesema wako katika mchakato wa kufika mikoa mingine inayokuwa sana katika soko la milki kama vile Tanga, Morogoro, Pwani na Mbeya huku nia ikiwa ni kufika nchi nzima.

 

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa kikao hicho kutoka kampuni ya GimcoAfrika Ltd Bw. Herien Muro amesema, elimu waliyopata kupitia kikao kazj ni muhimu kwa kuwa inaenda kuondoa udanganyifu huku ikiisaidia serikali kupata mapato.

 

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia kitengo cha Milki (REAL ESTATE)  inaendesha mijadala ya pamoja na wadau kwa lengo la kupata maoni kuhusu utambuzi na usajili wa wadau wa sekta ya milki ili kuboresha na kukuza sekta ya milki nchini.


 

‐----‐--------mwisho------------


Washiriki wa mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa wadau wa sekta ya milki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mjadala uliofanyika mkoani Arusha tarehe 12 Februari 2025.

Bw. Bariki Ileta kutoka Kitengo cha Milki Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwasilisha mada kwenye Mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa wadau wa sekta ya milki uliofanyika mkoani Arusha tarehe 12 Februari 2025.

Bw. Gerald Mboya kutoka kampuni ya Arusha Homes akichangia mada wakati wa mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa wadau wa sekta ya milki uliofanyika mkoani Arusha tarehe 12 Februari 2025.

Mwakilishi wa kampuni ya GimcoAfrika Ltd Bw.Herien Muro akichangia mada wakati wa mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa wadau wa sekta ya milki uliofanyika mkoani Arusha tarehe 12 Februari 2025.

Sehemu ya washiriki wa Mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa wadau wa sekta ya milki wakifuatilia uwasilishwaji mada wakati wa mjadala uliofanyika mkoani Arusha tarehe 12 Februari 2025.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Milki Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Wilson Wairara akizungumza wakati wa Mjadala kuhusu Utambuzi na Usajili wa wadau wa sekta ya milki uliofanyika Arusha tarehe 12 Februari 2025.

 (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link