Home » » Viongozi wa CCM waaswa kutokubali kutumika vibaya kwa kununuliwa na kupokea rushwa

Viongozi wa CCM waaswa kutokubali kutumika vibaya kwa kununuliwa na kupokea rushwa

Written By CCMdijitali on Wednesday, June 18, 2025 | June 18, 2025


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla



Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka viongozi wa CCM kutokubali kutumika vibaya kwa kununuliwa na kupokea rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.

Ameyasema hayo alipokutana na Viongozi wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Kamati za Siasa za Jimbo na wadi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama ndani ya Wilaya ya Kaskazini "B", Mkoa wa kaskazini ungaja katika Tawi la CCM Mahonda.

Amesema ni vyema kwa viongozi kuwa wazalendo kwa kuweka mbele maslahi ya chama na kuwa tayari kujitoa kwa hali na mali katika kukitumikia chama cha Mapinduzi.

Mhe. Hemed amesema kwa kipindi chote cha kuelekea uchaguzi Mkuu viongozi na wanchama wa CCM wanatakiwa kuwa wavumilivu na wastahmilivu na kuachana na mambo yote yanayokitia dosari chama ili kuwa mfano bora wa kuigwa na vyama vyengine.

Amesisitiza uminifu, uadilifu na kuacha utashi binafsi kwa viongozi na wajumbe watakaofanya kazi ya uteuzi wa wagombea jambo litakalopelekea kupata wagombea wenye sifa na uwezo wa kuwatetea majimboni mwao pamoja na kukiletea ushindi wa kishindo chama cha mapinduzi.

Mhe.Hemed amewataka wanachama wa CCM kufanya kazi kwa umoja na mshikamano katika kukijenga na kukiimarisha chama cha Mapinduzi hasa kipindi hiki muhimu cha kukipambia chama kiweze kushinda katika uchaguzi wa mwezi oktoba na kuebelea kushikilia dola.

Amesema cha Mapinduzi ni Chama cha wana CCM wote hivyo kila mmoja ana haki ya kugombea akiwa na sifa zinazokubalika ndani ya chama na kwa jamii iliyomzunguka.

Amewahamasisha wanawake na vijana kujitokeza kwa wingi katika kitumia haki yao ya kikatiba kwa kugombea nafasi mbali mbali ili waweze kukitumikia chama chao.

Katibu wa Idara ya Siasa, Itikadi, Uwenezi na Mafunzo ya chama ndugu Khamis Mbeto khamis amesema maendeleo makubwa yamefanywa na Serikali ya Awamu ya nane ikowemo ujezi wa miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo inaendelea kuwanufaisha wanachi wa Mkoa wa Kaskazini.

Mbeto amesema kuna kila sababu ya kuendelea kuwarejesha madarakani ifikapo Oktoba Rais Dkt Mwinyi na Rais Dkt samia ili waedelee kuiimarisha na kuijenga vyema Tanzania.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini "B" ndugu Ali Khamis Ali amesema wakati utakapofika wa kupitisha wagombea kamati hazitakwenda kinyume na matakwa ya katiba ya chama na watafanya kazi kwa haki uwazi na hakuna mgombea atakae onewa kila mtu atapewa haki yake anayostahiki.

Katibu Ali amesema wanachama wa CCM wa Wilaya ya Kaskazini "B" wanaahidi ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu na hawatopoteza jimbo hata moja ndani ya Mkoa huo.

Imetolewa na Kitengo cha Habari(OMPR)
Tarehe 14.06.2025

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link