Home » » BALOZI MUSSA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA

BALOZI MUSSA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA

Written By CCMdijitali on Friday, July 25, 2025 | July 25, 2025

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Dkt. Habib Kambanga, katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Kigali.

 

Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, hususan katika masuala yaliyojadiliwa kwenye Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) ngazi ya wataalam, pamoja na maandalizi ya hatua zinazofuata za mkutano huo.

 

Viongozi hao wameeleza dhamira ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki na kukuza ushirikiano katika maeneo ya kipaumbele kama vile biashara, miundombinu, usalama, nishati, kilimo na mawasiliano, kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

 

Balozi Mussa yupo nchini Rwanda kushiriki Mkutano wa 16 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda, unaofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 26 Julai 2025.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa (Kushoto)  na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Dkt. Habib Kambanga (kulia) katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Kigali.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini Kigali

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa (Kushoto)  na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Dkt. Habib Kambanga (kulia) katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Kigali.

 Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Dkt. Habib Kambanga

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link