Home » » DKT. SAMIA: NIWAHAKIKISHIE, MAANDAMANO PEKEE YA OKT. 29 NI KUPIGA KURA

DKT. SAMIA: NIWAHAKIKISHIE, MAANDAMANO PEKEE YA OKT. 29 NI KUPIGA KURA

Written By CCMdijitali on Tuesday, October 21, 2025 | October 21, 2025

𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗞𝗨𝗘𝗡𝗗𝗘𝗟𝗘𝗔 𝗞𝗨𝗜𝗙𝗨𝗡𝗚𝗨𝗔 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠 𝗞𝗪𝗘𝗡𝗬𝗘 𝗠𝗜𝗨𝗡𝗗𝗢𝗠𝗕𝗜𝗡𝗨 𝗬𝗔 𝗕𝗔𝗥𝗔𝗕𝗔𝗥𝗔 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗗𝗔𝗥𝗔𝗝𝗔

𝙈𝙧𝙖𝙙𝙞 𝙬𝙖 𝘿𝙈𝘿𝙋 𝙠𝙪𝙢𝙖𝙡𝙞𝙯𝙖 𝙘𝙝𝙖𝙣𝙜𝙖𝙢𝙤𝙩𝙤 𝙮𝙖 𝙢𝙖𝙛𝙪𝙧𝙞𝙠𝙤 𝘿𝙨𝙢.

Mgombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 amesema kuwa akipata ridhaa ya kuongoza tena nchi kwa miaka mitano ijayo, atahakikisha Serikali yake itajenga barabara za makutano (fly over) katika barabara za Morocco, Mwenge, Magomeni, barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Umoja wa Mataifa.

Dkt. Samia amesema sababu ya ujenzi huo ni kupunguza msongamano na kukuza shughuli za biashara katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ambapo zitaongeza tija katika ukuaji wa uchumi endelevu wenye kumgusa Mtanzania mmoja mmoja.

Akizungumza mbele ya kadamnasi ya wananchi wa Kinondoni na Ubungo alipokuwa akinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2025/30), sera na Ahadi zake katika viwanja vya Leaders Club, amesema atayakamilisha hayo pale ambapo wananchi watakwenda sambamba na kuchagau mafiga matatu kwa maana ya Rais kutoka CCM, Wabunge na Madiwani ili kuondoa makandokando katika kutekeleza majukumu hayo.

Pia, Mgombea Urais Dkt. Samia, ameahidi kujenga barabara ya Kimara - Mavurunza - Bonyokwa inayopita kwenye majimbo matatu ya Segerea, Ubungo na Kibamba yenye urefu wa kilomita 7 kwa kiwango cha lami huku akiongeza kuwa Serikali yake itatenga bajeti ili kujenga barabara nyingine muhimu kwa maendeleo ya wilaya zote zilizipo ndani ya Jiji la Dar es salaam.

Aidha, Dkt. Samia ameahidi kufanya utanuzi wa barabara ya Mwaikibaki yenye kilomita 9 kutoka Morocco - Kawe hadi Garden road pamoja na barabara ya Tegeta hadi Bagamoyo yenye urefu wa kilomita 57, Kibamba hadi Mloganzila yenye urefu wa kilomita 8.

Akigusia suala la changamoto ya mafuriko kwa baadhi ya maeno ya Jiji la Dar es salaam, Dkt. Samia amehaidi kuondoa changamoto hiyo katika kipindi cha mvua kwa maeneo mbalimbali ikiwemo yanayopakana na mto Gide, mto Mbezi na mto China akieleza kuwa changamoto hiyo itatatuliwa kupitia mradi wa pili wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP)

𝗛𝗔𝗞𝗨𝗡𝗔 𝗧𝗜𝗦𝗛𝗜𝗢 𝗟𝗔 𝗨𝗦𝗔𝗟𝗔𝗠𝗔 𝗟𝗜𝗧𝗔𝗞𝗔𝗟𝗢𝗞𝗨𝗪𝗘𝗣𝗢, 𝗡𝗘𝗡𝗗𝗘𝗡𝗜 𝗠𝗞𝗔𝗣𝗜𝗚𝗘 𝗞𝗨𝗥𝗔 - 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔

𝙈𝙖𝙩𝙪𝙨𝙞 𝙣𝙞𝙖𝙘𝙝𝙞𝙚𝙣𝙞 𝙢𝙞𝙢𝙞, 𝙣𝙞𝙣𝙖𝙮𝙖𝙗𝙚𝙗𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙣𝙞𝙖𝙗𝙖 𝙮𝙚𝙣𝙪.

"..Niwahakikishie tarehe 29, kesho kutwa tu mwezi huu wa 10, niwaombe tokeni muende mkapige kura."

"Ninayeongea hapa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hii, ninataka niwaambie, maandamano yatakayokuwepo ni ya watu kwenda vituoni kupiga kura, hakuna maandamano mengine yatakayokuwepo hapa.."

"..hakuna tishio la kiusalama litakalokuwepo, anayesemahapa ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi hii."

"Niwaombe ndugu zangu, twendeni mkapige kura, twendeni mkapige kura... Ndugu zangu mengine niachieni mimi, matusi niachieni mimi, ninayabeba kwa niaba yenu"

"Niliapa kuwa Rais wa Tanzania, niliapa kuilinda Nchi hii kwa kudumisha Amani, Umoja na Mshikamano wetu"

Hayo yamesemwa na Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 wakati akizungumza kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo tarehe 21 Oktoba 2025.

𝘾𝙃𝘼𝙂𝙐𝘼 𝙎𝘼𝙈𝙄𝘼, 𝘾𝙃𝘼𝙂𝙐𝘼 𝘾𝘾𝙈

DKT. SAMIA: TUTAHAKIKISHA DAR INAONDOKANA NA ADHA YA MAJI KWA MIRADI MIPYA


"Katika miaka mitano inayokuja, tutaendelea kukamilisha utekelezaji wa miradi ya Bwawa la Kidunda lenye thamani ya Shilingi bilioni 336, na bwawa hili la Kidunda litakwenda kuhudumia mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro. Lakini mradi wa pili tunaokwenda kuufanya ili kuondoa uhaba wa maji Dar es Salaam hasa wakati wa kiangazi, ni mradi mkubwa wa kutoa maji mto Rufiji ambao kazi ya upembuzi yakinifu na utafiti wa kina tayari tumekwishaianza na awamu hii tunakwenda kufanya utekelezaji ili Dar es Salaam ipate maji kutoka Kidunda, Ruvu na Mto Rufiji kuondoa kabisa kadhia ya uhaba wa maji", - Dkt. Samia.

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 21, 2025.


"Niwahakikishie tarehe 29, kesho kutwa tu mwezi huu wa 10, niwaombe tokeni muende mkapige kura. Ninayeongea hapa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hii, ninataka niwaambie, maandamano yatakayokuwepo ni ya watu kwenda vituoni kupiga kura, hakuna maandamano mengine yatakayokuwepo hapa, hakuna tishio la kiusalama litakalokuwepo, anayesema ni Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi hii. Niwaombe ndugu zangu, twendeni mkapige kura, twendeni mkapige kura... Ndugu zangu mengine niachieni mimi, matusi niachieni mimi, ninayabeba kwa niaba yenu", - Dkt. Samia.

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 21, 2025.

KUANZIA 2026 MTAONA MAGEUZI MAKUBWA YA MWENDOKASI DAR - DKT. SAMIA


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali yake itakwenda kusimamia na kukamilisha mradi wa miundombinu ya barabara ya mabasi yaendayo haraka maarufu kama mwendokasi, hiyo itafanyika ikiwa atachaguliwa kuiongoza nchi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Dkt. Samia ameyasema hayo akizungumza kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 21, 2025 ambapo amesisitiza kuwa utoaji wa huduma ya usafiri na usafirishaji kupitia miundombinu hizo zitakapokamilika, utajikita zaidi kwenye sekta binafsi.

"Tukapomaliza barabara zote, ni fursa muhimu kwa sekta binafsi kupata kazi ya kubeba abiria na kurudisha, kazi hiyo kwa kiasi hatutaki kuifanya sisi serikali bali sekta binafsi wataingiza mabasi yao na wafanye uendeshaji wa shughuli hizo", ameeleza Dkt. Samia.

Amewaahidi wakazi wa Dar es Salaam kuwa kuanzia Januari, 2026 kutakuwa na mageuzi makubwa ya utoaji wa huduma ya miundombinu ya mwendokasi.
Published from Blogger Prime Android App
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link