RAIS MWINYI AISHUKURU INDIA KWA MCHANGO MKUBWA KATIKA MAENDELEO YA ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameishukuru Serikali ya India kwa misaada ambayo imeku...
Latest Post
December 01, 2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameishukuru Serikali ya India kwa misaada ambayo imekuwa ikichangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Balozi wa India nchini, Balozi Bishwadip Dey, aliyefika Ikulu Zanzibar leo tarehe 01 Desemba 2025 kuwasilisha salamu maalumu za pongezi kufuatia ushindi alioupata katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Rais Dkt. Mwinyi ameihakikishia India kuwa Zanzibar itaendelea kuimarisha uhusiano wa karibu na wa muda mrefu baina ya nchi hizo mbili kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Ameeleza kuwa misaada inayotolewa na India kwa Zanzibar katika sekta za miundombinu, mradi wa maji mjini, nafasi za mafunzo kwa vijana wa Zanzibar, afya na teknolojia ya mawasiliano imekuwa kichocheo muhimu cha kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo mawili na kuchangia maendeleo katika nyanja tofauti.
Aidha, Dkt. Mwinyi amesema Zanzibar inafarijika na ushirikiano inaoupata kutoka Serikali ya India na ipo tayari kwa ushirikiano zaidi hususan katika sekta za biashara, elimu na afya.
Ameipongeza India kwa kuendelea kutoa nafasi za mafunzo kwa vijana wa Zanzibar katika nyanja mbalimbali.
Rais Dkt. Mwinyi amemueleza Balozi Bishwadip kuwa zipo fursa zaidi za uwekezaji ambazo wawekezaji na wafanyabiashara wa India wanaweza kuwekeza hapa nchini, na amewakaribisha kuwekeza hususan katika sekta za utalii na uchumi wa buluu ambazo ndizo sekta kuu za uchumi wa Zanzibar.
Akizungumzia teknolojia ya habari na mawasiliano, Rais Dkt. Mwinyi amesema mafunzo na maendeleo ya teknolojia yanayotolewa katika Taasisi ya IIT Madras hapa nchini yamekuwa chombo muhimu katika kuiwezesha Zanzibar kufikia dhamira ya kuwa na huduma za kidijitali katika sekta zote za utoaji huduma, na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano zaidi kwa ajili ya maendeleo ya taasisi hiyo.
Naye Balozi Bishwadip Dey amesema India itaendelea kushirikiana na Zanzibar katika nyanja mbalimbali za maendeleo kwani uhusiano huo ni nguzo muhimu ya kudumisha na kuimarisha mahusiano ya muda mrefu baina ya mataifa hayo.
Amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa uongozi wake unaoleta mabadiliko makubwa ya maendeleo na kuihakikishia Zanzibar misaada zaidi, nafasi za mafunzo nchini India na ongezeko la bajeti ya miradi ya maendeleo.

RAIS MWINYI AISHUKURU INDIA KWA MCHANGO MKUBWA KATIKA MAENDELEO YA ZANZIBAR
Written By CCMdijitali on Monday, December 1, 2025 | December 01, 2025

Labels:
ZANZIBAR