MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
Latest Post
October 25, 2015
Katibu Mwenezi CCM Arusha, atimiza haki yake ya kikatiba ,Kaloleni,Arusha.
Written By CCMdijitali on Sunday, October 25, 2015 | October 25, 2015
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akisubiri kutimiza haki yake ya kikatiba, ili kuweza kumchagua Kiongozi anayemtaka, leo katika kituo cha Kupigia kura Kaloleni Magharibi, Jijini Arusha.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akitimiza haki yake ya kikatiba, ya kumchagua Kiongozi anayemtaka, leo katika kituo cha Kupigia kura Kaloleni Magharibi, Jijini Arusha.
Baadhi ya Wasimamizi na wapiga kura katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya kaloleni leo.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akionyesha alama ya wino mara baada ya i kutimiza haki yake ya kikatiba, ya kumchagua Kiongozi anayemtaka, leo katika kituo cha Kupigia kura Kaloleni Magharibi, Jijini Arusha.
Labels:
ARUSHA
October 25, 2015
JIJI LA MWANZA LAGUFULIKA ,YAFUNGA KAMPENI ZAKE KWA KISHINDO
Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa hitimisho la kampeni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa hitimisho la kampeni.
Umati wa maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza walifika kuhudhuria uwanja wa CCM kirumba katika hitimisho la Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea machache mtambulisha ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa hitimisho la kampeni.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akimnadi Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wa pili kutoka kulia, Mgombea Mwenza Mama Samia Hassan Suluhu na wagombea ubunge wa majimbo ya Ilemela Anjela Mabula wa kwanza kushoto na Stanslaus Mabula Nyamagana wa tatu kutoka kushoto
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akimnadi Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wa pili kutoka kulia,na wagombea ubunge wa majimbo ya Ilemela Anjela Mabula wa kwanza kushoto na Stanslaus Mabula Nyamagana wa tatu kutoka kushoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwanadi wagombea ubunge wa Mwanza.Kulia ni mgombea wa Ubunge wa jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula na mgombea wa Ubunge wa jimbo la Ilemela Anjela Mabula.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiburudika na Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli pamoja na wanakibajaji ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa hitimisho la kampeni.
Umati wa maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza wakifuatilia kufungwa kampeni za chama cha Mapinduzi CCM katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mgombea Mwenza Mama Samia Suhulu, akipokelewa ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa hitimisho la kampeni.
Wanakibajaji nao hawakuwa nyuma.
Chege na Temba wakitoa burudani.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimia na Kada wa CCM, Wema Sepetu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa hitimisho la kampeni.
Makada wa CCM, Steve Nyerere na Wema wepetu wakiongea ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa hitimisho la kampeni.
Kazi ni Kazi.... Asha bokooooo akionyesha umahili wa kupiga PUSH UPS....
Asha boko katika ubora wake.
Wema Sepetu katika ubora wake.
Rais ni Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea machache mtambulisha ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati wa hitimisho la kampeni.
Ujumbe!
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli akitoa sera zake kwa wananchi waliofika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati ufungaji wa kampeni.
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli akiwa na mgombea wa Ubunge wa jimbo la Nyamagana L. Mabula.
Umati wa maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza walifika kuhudhuria uwanja wa CCM kirumba katika hitimisho la Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli akiingia uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati ufungaji wa kampeni.
Mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli akisindikizwa kuingia uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati ufungaji wa kampeni.
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan akisalimia wananchi wakati akiingia ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati ufungaji wa kampeni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiingia uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati ufungaji wa kampeni.
Labels:
KITAIFA
October 25, 2015
Balozi Seif akizungumza na vyombo vya Habari mara tuu bada ya kumaliza kutumia haki yake ya kupiga kura hapo Skuli ya Sekondari ya Kitope ambapo ndio kwenye kituo chake cha uchaguzi.
Picha na –OMPR – ZNZ.
Balozi Seif apiga kura ya Kumchagua Rais wa Zanzibar, Mwakilishi pamoja na Diwani kwenye uchaguzi Mkuu
Baadhi ya Wananchi katika vituo mbali m bali vya kupigia kura wakihakiki majina yao kwa hatua ya mwisho kabla ya kupanga foleni kwa ajili ya kupiga kura kuwachaguwa viongozi wao watakaowaoongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Baadhi ya Wananchi wakiwa katika msururu kwa ajili ya kupiga kura ya
kuwachangua Marais, Wabunge, wawakilishi na Madiwani hapo katika kituo
cha kupiga kura skuli ya Sekondari Kitope Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa
wa Kaskazini Unaguja.
Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Tiketi ya CCM
Jimbo la Mahonda ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi akiwa katika foleni ya kusubiri kupiga kura kwenye Kituo
chake kiliopo Skuli ya sekondari ya Kitope.
Balozi Seif akipiga kura ya Kumchagua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mbunge wa Bunge ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika
Kituo chake hapo Skuli ya Sekondari ya Kitope.
Mgombea nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Mahonda kwa Tiketi ya CCM
Balozi Seif akipiga kura ya Kumchagua Rais wa Zanzibar, Mwakilishi
pamoja na Diwani kwenye uchaguzi Mkuu hapo Skuli ya Sekondari Kitope.
Karani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ambae jina lake halikupatikana akimueka alama Balozi Seif kuashiria kwamba ameshakamilisha zoezi la Kupiga kura ya kumchagua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Mbunge, Mwakilishi na Diwani.
Balozi Seif akizungumza na vyombo vya Habari mara tuu bada ya kumaliza kutumia haki yake ya kupiga kura hapo Skuli ya Sekondari ya Kitope ambapo ndio kwenye kituo chake cha uchaguzi.
Picha na –OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Hatimae ile siku ya Jumapili ya Tarehe 25 Oktoba ambayo Watanzania walikuwa wakiisubiri kutoa maamuzi ya kutumbukiza kura ili kukipa dhamana chama kilichonadi vyema sera na Ilani yake na kukubalika imetimia.
Watanzania hao wamepata fursa ya kutimiza haki yao ya kidemokrasia ya kuwachagua viongozi watakaowaongoza katika kipindi cha miaka mitano ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa ulioanza mwaka 1995 takriban chaguzi Tano sasa.
Wapiga kura wa upande wa Tanzania Bara waliokuwa chini ya usimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
{ NEC } wamewajibika kupiga kura kwa nafasi Tatu za Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Ubunge na Udiwani wakati wale wa Zanzibar wamepiga kura kwa nafasi Tano za Urais wa Muungano, Ubunge,Urais wa Zanzibar,Uwakilishi pamoja na Udiwani.
Moja kati ya jambo lililoleta faraja ndani ya vituo vya wapiga kura Mjini na Vijijini ni ile hali ya amani na usalama iliyotanda ambayo ilikuwa ikisisitizwa kulindwa na kudumishwa wakati wa Kampeni za uchaguzi zilizochukuwa takriban mwezi mmoja.
Viongozi mbali mbali pamoja na maelfu ya wananchi walijitokeza mapema asubuhu kupiga kura na kutimiza ile kiu yao iliyowashika tokea kuanza kwa zoezi ya kura za maoni, uandikishaji wa daftari la wapiga kura, kampeni hadi upigaji kura wenyewe.
Misururu mirefu ya Wananchi iliyowekwa kwa mujbu wa mfumo wa majina ya wapiga kura ilianza mapema alfajiri mara tuu baada ya wale wananchi waumini wa dini ya Kiislamu kutoka misikitini kutekeleza Ibada ya sala ya Asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Sheni na Mkewe Mama Mwanamwema Shein walipiga kura katika Kituo chao cha kupiga kura cha Kijiji cha Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi wakapiga kura katika Kituo chao kiliopo Skuli ya Sekondari ya Kitope Jimbo la Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja saa 2.25 za asubuhi.
Balozi Seif pia ni mgombea wa nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika Jimbo hilo jipya la Mahonda kwa mujibu wa mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kufuatia ongezeko na idadi ya watu kwa mujibu wa Sensa ya Idadi ya watu na Makaazi ya mwaka 2012.
Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kupiga kura Balozi Seif alisema ameridhika na zoezi zima liloanza mapema asubuhi ambapo wananchi mbali mbali tayari wameshatumia haki yao ya kupiga kura na kurejea nyumbani kuendelea na shughuli zao za kimaisha.
Balozi Seif aliwaomba wananchi kuepuka kukaa vituoni kwa ushawishi wa kutaka kulinda kura kwani ni vyema suala hilo likaachiliwa Mahkama kutoa uamuzi kwa vile tayari liko mahakamani.
Akigusia suala la mawakala wa vyama Balozi Seif akiwa mgombea wa nafasi ya Uwakilishi jimbo la Mahonda aliwaomba wagombea wenzake wakazingatia sheria na kanuni za Tume ya Uchaguzi ya kuweka mawaka wanaoishi katika maeneo ya kupiga kura ili kusimamia kura zao.
Alisema kitendo cha baadhi ya wagombea hao kuweka mawaka wanaoishi nje ya vituo vyao vya kupiga kura mbali ya kwenda kinyume na sheria ya Tume ya chaguzi lakini pia kinaweza kuleta vurugu zisizo na msingi wowote.
“ Makawala wanaosimamia wagombea wa uchaguzi lazima wanatakiwa wawe wakaazi wa eneo la kupigia kura kwa mujibu wa sheria na kanuni za Tume ya Uchaguzi “. Alisema Balozi Seif.
Moja kati ya jambo lililoleta faraja kubwa ndani ya zoezi zima la upigaku kura ni ile hali ya amani miongoni mwa wapiga kura katika vituo mbali mbali vya wapiga kura Mjini na Vijijini.
Mmoja kati ya wapiga kura katika kituo cha kupiga kura cha Skuli ya Sekondari ya Kitope ambae alikataa kutaja jina lake alisema ameridhika na maandalizi mazima yaliyofanywa na Tume za Uchaguzi za Taifa na Ile ya Zanzibar na kuwapa fursa wananchi kutekeleza haki yao katika misingi ya utulivu na bila ya usumbufu.
Alisema yule mwananchi atakayefikia maamuzi ya kutaka kuzilaumu Tume za Uchaguzi ajijue kwamba ana matatizo kwa vile fursa ilitolewa mapema kwa wananchi kuangalia majina yao kwa karibu siku nne kabla ya uchaguzi na akapewa nafasi ya kutoa taarifa ili afanyiwe marekebisho endapo jina lake hakuliona.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
25/10/2015.
Labels:
KITAIFA
October 24, 2015
Wa kwanza kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Nd. Vuai Ali Vuai na kulia ya Balozi Seif ni Spika wa Baraza la Wawakilishi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mh. Pandu Ameir Kificho.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri u ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa Taarifa ya hali ya CCM ilivyo katika kuelekea kwenye ushindi wa uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho.
Balozi Seif alisema kazi kubwa iliyofanywa na washirika hao imewafanya Wananchi walio wengi kuelewa sera na ilani ya vyama vya Kisiasa na kupelekea kuwa watulivu muda wote licha ya baadhi ya Viongozi wa Kisiasa kuanza ishara ya kutaka kuparaganya Wananchi.
Alisema kutokana na harakati za maandalizi ya uchaguzi Mkuu kuanzia mchakato wa kura za maoni Chama cha Mapinduzi Mwaka huu kinatarajia kufanya vizuri zaidi baada ya kuridhika na mahudhurio makubwa ya Wanachama wake pamoja na Wananchi wakati wa kufuatilia Sera na Ilani zake.
Balozi Seif alifahamisha kwamba tathmini ya kina iliyofanywa na wataalamu wa Chama chake umeelezea kwamba CCM itashinda kwa zaidi ya asilimia 60% katika nafasi ya Urais wa Zanzibar na Asilimia 70% kwa nafasi za majimbo ya Zanzibar na kutarajia kuweka rikodi mpya tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya Kisiasa Nchini Tanzania.
Alisema viongozi wa upande wa vyama vya upinzani wanaelewa vyema uwezo huo wa CCM kushinda uchaguzi hali iliyowafanya waanze kuingiwa na wasi wasi na kufikiria mawazo ya kutaka kushawishi vijana wao waandae mipango ya kufanya vurugu.
Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Kampeni ya Taifa ya Uchaguzi ya CCM Zanzibar aliwaeleza Wana Habari hao kwamba Wananchi wa Zanzibar wamepata mafanikio makubwa katika miradi yao ya maendeleo na kiuchumi kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Alisema Ilani hiyo ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010 hadi 2015 imefikia utekelezaji wake kwa asilimia 98% kiasi kinachowafanya Wananchi wengi kuendelea kukiamini katika kuwaletea maendeleo yao.
Balozi Seif alifahamisha kwamba Ilani ya Chama cha Mapinduzi inayoanzia mwaka huu wa 2015 hadi 2020 ambayo imenadiwa vyema kwa wananchi katika mikutano mbali mbali ya Kampeni imeonyesha ishara bora ya Matumaini kwa Wananchi walio wengi.
Akijibu swali kuhusu Changamoto endapo Kamati yake ya Kampeni ya Uchaguzi Taifa ya CCM ilipambana nayo Balozi Seif alielezea faraja yake kwamba kazi kubwa iliyofanywa ndani ya ilani mpya ndio iliyofanikisha kazi yao kuwa ya mafanikio.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba Wananchi wote kujitokeza kwa wingi kuitumia haki yao ya kidemokrasia katika kupiga kura kwa kuwachagua Viongozi watakaowaongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Aliwataka Wananchi wote wasivae sare wala vitu vinavyoonyesha alama za vyama vya siasa wakati wanapokwenda vituoni kupiga kura kwa vile kitendo hicho kitakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria za Uchaguzi.
Alisema Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi imejiandaa vya kutosha katika kukabiliana na vurugu zozote zitakazojitokeza wakati wa kupiga kura, Kuhesabu na kumalizia matokeo ya uchaguzi huo.
Chama cha Mapinduzi kilizindua Kampeni zake za Uchaguzi Tarehe 13 Septemba mwaka 2015 kwa upande wa unguja na Tarehe 15 Septemba kwa upande wa Pemba wakati Kampeni hizo zilizmalizia Tarehe 22 Oktoba kwa Pemba na Tarehe 23 Oktoba kwa Unguja.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
24/10/2015.
Balozi Seif atoa Taarifa ya hali ya CCM kuelekea ushindi uchaguzi Mkuu 2015
Written By CCMdijitali on Saturday, October 24, 2015 | October 24, 2015
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Taifa ya CCM Zanzibar Balozi Seif Al Iddi akitoa Taarifa ya hali ya CCM ilivyo katika muelekeo wake wa safari ya ushindi katika uchaguzi Mkuu mbele ya vyombo mbali mbali vya Habari hapo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
Wapiga pich wa vyombo mbali mbali vya Habari wakiwa kazini kurikodi Taarifa ya safari ya CCM katika uchaguzi Mkuu iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Taifa ya CCM Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi Seif kati kati akijibu maswali ya wana Habari mbali mbali mara baada ya kutoa Taarifa ya safari ya CCM katika kushinda uchaguzi Mkuu aliyoitoa hapo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Wa kwanza kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Nd. Vuai Ali Vuai na kulia ya Balozi Seif ni Spika wa Baraza la Wawakilishi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mh. Pandu Ameir Kificho.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Wananchi ,Wafuasi wa vyama vya Siasa , Waandishi wa Habari,Wasanii pamoja na Taasisi za kiraia Nchini wamepongezwa kwa jitihada walizochukuwa za kuifanya Nchi kuendelea kubakia katika hali ya amani na Utulivu ndani ya kipindi choche cha mchakato wa wagombea na maandalizi ya kampeni za uchaguzi zilizokuwa zikiendelea katika maeneo mbali mbali nchini.