Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Msanii Fadhil Mungi wa kikundi cha ngoma cha Meatu wakati alipowasili na kupokelewa na uongozi wa Chama Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu katika kata ya Itinje Kijiji cha Itinje. Baada ya kuwasili katika wilaya hiyo, moja kwa moja ameanza ziara yake kwa ajili ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo huku akihimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, lengo kuu la ziara hiyo ni kuhakikisha serikali inatekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho ili kuwaletea wananchi maendeleo, Katika ziara hiyo Abdulrahman Kinana ameongoza na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye. Katibu mkuu huyo atakuwa na ziara ya siku 5 katika mkoa huo wa Simiyu kabla ya kuanza ziara nyingine ya siku 6 mkoani Mara.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Pascal Mabiti kulia wakiongozana na Msanii Fadhil Mungi wakati katibu Mkuu huyo akielekea kufungua moja ya shina katika kata hiyo ya Itinje.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk Titus Kamani wakati alipokuwa akizungumza na wananchi ili kumakaribisha baada ya kuwasili katika wilaya ya Meatu, kulia ni Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi
Ndugu Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa CCM kata ya Ngoboko mara baada ya kushiriki shughuli za ujenzi wa jengo hilo.
Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM ndugu Nape Nnauye katikati Mh. Luhaga Mpina Mbunge wa Jimbo la Kisesa na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Ndugu Dk Titus Kamani wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman wakati alipokuwa akizungumza na wanaCCM wa Kata ya Ngoboko.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wana Itinje mara baada ya kuwasili na kupokelewa katika wilaya hiyo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga ripu katika jengo la ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kata ya Ngoboko, huku Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akishuhudia tukio hilo.