Mkuu wa mkoa wa ARUSHA, DAUDI NTIBENDA
Mkuu wa mkoa wa ARUSHA, DAUDI NTIBENDA ameziagiza halmashauri za wilaya za mkoa huo kutenga fedha kwa ajili ya mabaraza ya biashara ya wilaya ili kuyawezesha mabaraza hayo kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
NTIBENDA ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la biashara la mkoa wa ARUSHA amesema mabaraza la biashara ya wilaya yanahitaji kutengewa fedha kwenye bajeti za halmashauri za wilaya ili yaweze kuchochea ukuaji wa shughuli za biashara na uwekezaji mkoani humo.
Naye Mkurugenzi wa Mazingira ya Biashara wa Baraza la Taifa la Biashara –TNBC- ARTHUR MTAFYA amesema kunahitajika kuwepo kwa mawasiliano ya mara kwa mara kati ya sekta binafsi na sekta ya umma, kuibua fursa za kibiashara na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye mikoa .