Home » » Maofisa wa ARSENAL kuja nchini

Maofisa wa ARSENAL kuja nchini

Written By CCMdijitali on Thursday, January 15, 2015 | January 15, 2015


MAOFISA kutoka katika klabu ya ARSENAL ya UINGEREZA wamepanga kuja nchini kwa ajili ya kujadili fursa za ushirikiano na wafanyabiashara kadhaa wa hapa nchini. 

Huu utakuwa ujumbe wa kwanza kwa klabu hiyo kuja kujenga ushirika katika maeneo ya masoko na chapa zake, ili kutanua mafanikio yaliyofikiwa kwenye nchi nyingine za Afrika kama Kenya, UGANDA na NIGERIA. 

Ofisa Biashara Mkuu wa ARSENAL, VINAI VENKATESHAM amesema wameichagua TANZANIA kwa sababu wanajua wana mashabiki wengi, na kwa kushirikiana na taasisi za TANZANIA, watakuwa karibu zaidi na mashabiki wao kuliko ilivyokuwa awali. 

Ujumbe huo uanatarajia kuwasili nchini Januari 18 mwaka huu, ambapo watakaa kwa wiki moja jijini DSM kuitisha mikutano kadhaa ya awali ya kibiaashara na kuzindua rasmi mchakato wa kutafuta washirika wa kwanza kabisa nchini.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link