Balozi Seif akijumuika pamoja na Vijana Chipukizi pamoja na baadhi ya Viongozi wa UVCCM kwenye chakula cha mchana aliyowaandaliwa baada ya kazi ngumu waliyoifanya Vijana hao ya kushiriki matembezi ya kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka jana.
Makamu Mkuu wa Chipukizi wa UVCCM Zanzibar PiliHassan Suluhu akimpongeza Balozi Seif kwa kutimiza ahadi yake aliyoitowa kwao mwaka uliopita ya kula nao pamoja katika chakula cha mchana.
Baadhi ya Vijana Chipukizi wa UVCCM wakimsikiliza Balozi Seif hayupo pichani wakati akiwapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kulitumikia Taifa hili wakiwa na umri mdogo.
Balozi Seif akizungumza na Vijana Chipukizi wa UVCCM Mara baada ya kiula nao chakula cha mchanga hapo kwenye ukumbi wa CCVM Maisara Mjini Zanzibar.
Mke wa Balozi Seif Mama
Asha Suleiman Iddi akibadilishana mawazo na Vijana Chipukizi wa UVCCM
kwenye chakula cha mchana kilichoandaliwa na Balozi Seif hapo Maisara.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM
Balozi Seif Ali Iddi alisema Vijana Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM wana wajibu wa kukataa kuyumbishwa au
kudanganywa na watu wanaopenda kuwatumia wenzao kwa kutekeleza matakwa yao
binafsi.
Balozi Seif alisema hayo wakati wa chakula cha mchana alichowaandaliwa Chipukizi hao
kutekeleza ahadi aliyowapa ya kula nao pamoja baada ya kazi kubwa waliyoifanya
wakati wa matembezi ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar hapo Mwaka
jana.
Hafla hiyo ya chakula cha mchana ilifanyika katika ukumbi
wa CCM {CCM Social Hall } Maisara Mjini
Zanzibar na kuhudhuriwa pia na Viongozi wa ngazi ya juu ya Umoja wa Vijana wa
CCM Taifa.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alisema Chipukizi wa umoja wa Vijana wa CCM ndio wanajenga mazingira mazuri ya
nguvu na ushindi wa Chama cha Mapinduzi katika chaguzi zinazofanyika hapa
Nchini.
Aliwashukuru Vijana hao wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa
CCM kwa kupuuza kauli na ushawishi wanaopewa na baadhi ya Viongozi wa Siasa na
hata watu binafsi wanaopenda fitna zinazowagawa wananchi.
Aliwaasa Vijana hao kuendelea kupendana, kushikamana na
kushirikiana katika shughuli na harakati zao kwani hiyo ndio misingi imara
iliyowekwa ndni ya Chama cha Mapinduzi.
- “ Ningekuombeni msikubali kuyumbishwa wala kudanganwa lazima muwe makini kwani nyinyi ndio viongozi bora wa hapo baadaye “. Balozi Seif aliwasisitiza Vijana hao wa Chipikizi.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa alielezea faraja yake
kutokana na msimamo wa vijana hao
uliopelekea kufanikiwa vyema katika utii maadili ya Taifa pamoja na
Viongozi wao.
Mapema Makamu Mkuu wa Chipukizi Zanzibar Pili Hassan Suluhu
alimpongeza Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi
Seif kwa uungwana wake wa kutekeleza ahadi aliyowapa.
Pili Hassan kwa niaba
ya chipukizi wenzake amemuomba Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM
kulifikisha ombi lao kwenye Uongozi wa Juu wa CCM la kuomba washiriki
katika sherehe za maadhimisho ya kutimia miaka 33 okea kuundwa kwa chama cha
Mapinduzi mwaka 1977.