Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mh. Nasso Ahmed Mazrui na kushoto yake ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Baisra Tanzania { Tantrade } Bibi Jackline na Naibu Waziri wa Biashara Zanzibar Mh. Thuwaiba Kisasi.
Ofisa Kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bibi Robi Bwire akimpatia maelezo Balozi Seif wakati akikagua mabanda ya maonyesho kwenye Tamasha la Biashara.
Wa kwanza kushoto kulia ni Afisa wa Habari na Mawasiliano wa Wizara hiyo Bwana Othman Maalima Othman.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maendeleo ya Baisra Tanzania { Tantrade } Bibi Jackline na Waziri
wa Biashara Zannzibar Mh. Mazrui wakifurahia bidhaa za Miti shamba kwenye banda
la Maonyesho la Uganda.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
ametoa wito kwa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar kuanzisha eneo maalum kwa maonyesho ya
biashara kwa lengo la kutanua zaidi uhusiano wa kibiashara kati ya Zanzibar na
Mataifa mengine Duniani.
Alisema maonyesho ya Kibiashara siyo tu yanavutia na
kushawishi wawekezaji lakini pia huongeza ushirikiano karibu baina ya
wafanyabiashara wenyewe kwa wenyewe .
Balozi Seif alitoa wito huo wakati akilifungua tamasha la
Pili la Biashara la mwaka 2015 la maadhimisho ya kutimia miaka 51 ya Mapinduzi
ya Zanzibar linalofanyika katika uwanja wa mishezo wa Maisara Mjini Zanzibar.
Alisema lengo kuu la Tamasha la biashara Zanzibar ni kushajiisha ukuaji wa biashara kwa azma ya
kuirejeshea Zanzibar hadhi yake ya kuwa kituo cha biashara katika mwambao wa
Afrika Mashariki kwa karne kadhaa zilizopita.
Balozi Seif alifahamisha kwamba uwepo wa matamasha kama haya
Zanzibar hutoa fursa kwa wageni kujipangia muda wa kutembelea Zanzibar kwa
mapumziko pamoja na kujipatia mahitaji yao ya bidhaa tofauti zinazozalishwa
ndani na hata kwa zile Taasisi za nje zinazoshiriki maonyesho hayo.
Alisema wafanyabiashara
pamoja na wajasiri amali wanapaswa kuitumia vyema fursa hiyo adhimu ya
tamasha la biashara ili wakuze biashara zao kwa vile ni moja kati ya sekta
muhimu ya kukuza uchumi na kutoa ajira kwa wananchi walio wengi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali itaendelea
kushirikiana na wafanyabiashara wa pande zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania na Afrika Mashariki katika kuhakikisha sekta ya biashara inazidi
kukua sambamba na matamasha ya biashara
ili kuongeza idadi ya wageni.
Balozi Seif
alisisitiza umuhimu wa matamasha kama haya ya biashara kujumuishwa pia
maonyesho ya utamaduni wa Mzanzibari kama kazi za sanaa ya mkononi, vyakula vya
mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki na Muziki ambao unaonekana kutoweka katika
Historia kutokana na mabadiliko ya utandawazi.
Aliwaomba wafanyabiashara kuziepuka bidhaa zilizo chini ya
kiwango kwani kufanya hivyo kutamfanya mnunuzi wa bidhaa zao kupoteza fedha
bure pamoja na kuharibiwa mipango yake.
Balozi Seif alieleza kwamba Serikali imeanzisha Taasisi
inayosimamia viwango kwa lengo la kukuza ubora wa bidhaa zinazozalishwa pamoja
na zile zinazoagiziwa nje ya nchi masuala ambayo yanakwenda sambamba na
mikakati ya kuwasaidia wjasiri amali wa Zanzibar katika kufikia viwango
vinavyokubalika katika masoko ya Kimataifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Wizara ya
Biashara Zanzibar kwa kushirikiana na mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
{ Tantrade } pamoja na Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar kwa wazo lao la
pamoja la kuanzisha na kuendeleza Tamasha la Biashara hapa Zanzibar.
“ Na hili ni tamasha la Pili huku tukisherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Januari mwaka 1964 lengo likiwa kushajiisha ukuaji wa biashara kwa azma ya kuirejeshea Zanzibar hadhi yake ya kuwa kituio cha Biashara Mwambao wa Afrika Mashariki “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Mamlaka ya
Maendeleo ya Baisra Tanzania { Tanzania Trade Development Authority – Trade }
kwa uamuzi wake wa kuisaidia Wizara ya
Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar katika taaluma ya Maonyesho na matamasha ya
Baishara.
Balozi Seif aliitaka Mamlaka hiyo kuendelea kuiunga mkono
Zanzibar katika sekta hiyo ili ifikie hatua ya kujiendesha yenyewe katika sekta
hiyo muhimu ya Uchumi wa Taifa.
Aliwashukuru washiriki wa wa tamasha hili la Biashara
Zanzibar kutoka ndani na nje ya Nchi, Taasisi za Umma na zile Binafsi,
Mapampuni kwa kushiriki kwenye tamasha
la mwaka huu na kuwaomba washiriki kwenye matamasha yanayokuwa yanaandaliwa
hapa Zanzibar.
Mapema Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mh.
Nassor Ahmed Mazrui alisema ukuaji wa sekta ya B iashara hapa Nchini umeongeza
mapato ya nchi sambamba na huduma za fedha.
Waziri Mazrui alisema Tamasha la Biashara la Mwaka huu
limeshirikisha zaidi ya Makampuni 160 katika ya 200 yaliyoomba kushiriki
katika Tamasha hili kutoka Tanzania Bara
na wenyeji Zanzibar yakiwemo Makapumi
mawili ya Kigeni.
Alifahamisha kwamba mbali ya bidhaa mbali mbali zitakazouzwa
na kuonyeshwa kwenye Tamasha hilo la bishara lakini pia huduma za Michezo ya
Watoto itakuwepo ili kuwapa fursa watoto watakaotembelea Tamasha hilo kupata
burdani.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko aliwapongeza washiriki
wa Tamasha la kwanza la mwaka J ana
lililofanikiwa vyema kutokana na kukusanya mapato zaidi hya shilingi Milioni
220,630,150/- kutokana na bishara za papo kwa papo.
Alisema Tamasha la mwaka pia lilipokea maombi ya wateja
kutoka makampuni na watu binafsi kwa ajili hya kupata huduma zenye gharama ya
zaidi ya shilingi Milioni 90,000,000/=.
Tamasha la Pili la Biashara la mwaka 2015 la maadhimisho ya
kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar limeanza Tarehe 7 Januari mwaka huu
wa 2015 na kuendelea hadi Tarahe 13 Mwezi huu.