Bei ya mafuta yashuka
Written By CCMdijitali on Thursday, January 8, 2015 | January 08, 2015
Mkurugenzi mkuu wa EWURA, FELIX NGAMLAGOSI
Kasi ya kushuka kwa bei ya mafuta nchini Tanzania ni ndogo ikilinganishwa na ile ya soko la dunia jambo ambalo limesababisha watanzania kuendelea kununua mafuta ya petrol, dizeli na mafuta ya kwa bei kubwa.
Katika soko la dunia bei ya mafuta yasiyosafishwa imeshuka kwa kasi ya zaidi ya asilimia 43 kuanzia mwezi Julai mwaka jana hadi sasa, lakini hapa Tanzania bei ya mafuta yaliyosafishwa yameshuka kwa kasi ya chini ya asilimia 10.
Akizungumzia hali hiyo Mkurugenzi mkuu wa EWURA, FELIX NGAMLAGOSI amesema bei ya mafuta hapa nchini inaonekana bado ni kubwa kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi, gharama za usafirishaji na kodi za serikali ambazo hazijabadilika.
Amesema bei ya petrol imeshuka kwa shilingi 311 ambazo ni sawa na asilimia 16, diseli imeshuka kwa shilingi 244 ambazo ni sawa na asilimia 13 na bei ya mafuta ya taa imeshuka kwa shilingi 200 ambayo ni sawa na asilimia 11.
Labels:
BIASHARA