Magreth Chacha
Benki ya wanawake Tanzania -TWB -imeanzisha mikopo ya ufugaji kwa ajili ya wajasiriamali wanaojishughulisha na ufugaji wa kuku wa nyama au mayai.
Akizungumza mara baada ya kutembelea mashamba ya kuku ya wajasiriamali katika eneo la Madale jijini DSM, mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Magreth Chacha amesema mikopo hiyo inatolewa kwa wafugaji walioko kwenye vikundi au mjasiriamali mmoja mmoja .
Naye mratibu wa mafunzo ya wajasiriamali ya ufugaji bora wa kuku Green Mosh na kurugenzi wa shamba la kuku la TWIGA FEEDS Afred Mosh wamesema wajasiriamali wengi wanashindwa kuanzisha miradi ya ufugaji wa kuku kutokana na ukosefu wa mitaji.