DIAMOND PLATNUM
Mshindi wa tuzo 3 za CHANEL O 2014, NASIBU ABDUL maarufu DIAMOND PLATNUM anatumbuiza katika tuzo za 23 za mwana soka bora wa AFRIKA za mwaka 2014 zinazofanyika LAGOS, NIGERIA akiwa mwanamuzika pekee kutoka ukanda wa AFRIKA MASHARIKI.
Wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni mshindi mara tatu, YAYA TOURE kutoka mabingwa ligi ya ENGLAND MANCHESTER CITY, mshambuliaji wa timu ya BORUSSIA DORTMUND, na kipa wa timu ya NIGERIA VINCENT ENYEAMA.
Wachezaji walishinda tuzo hiyo mara nyingi zaidi kuanzia mwaka 1992 hadi 2013 ni SAMUEL ETO’O wa CAMEROON ambaye ameshinda mara nne, mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010, Toure ya IVORY COAST aliyeshibnda mara tatu mwaka, 2011, 2012, 2013, na mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya SENEGAL , EL HADJI DIOUF aliyenyakua tuzo hiyo mara mbili mwaka 2001 na 2002.