Home » » KAMATI KUU YA CCM YAMALIZA KIKAO CHA KAWAIDA.

KAMATI KUU YA CCM YAMALIZA KIKAO CHA KAWAIDA.

Written By CCMdijitali on Tuesday, January 13, 2015 | January 13, 2015

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya  Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza jambo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu Adam Kimbisa,wakati akitoka nje mara baada ya kumaliza kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa usiku huu,kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja,Zanzibar,kikao hicho kilianza mnamo majira ya saa sita mchana na kumalizika usiku mnamo saa mbili na dakika kadhaa mambo mbalimbali yakiwa yamejadiliwa ikiwemo suala la sakata la Akaunti ya Escrow,Hali ya kisiasa nchini,uchaguzi Mkuu na mambo ya Maadili na mengineyo.
Pichani ni Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na  Wanahabari usiku huu baada ya kikao cha kamati kuu cha CCM kuisha nje ya ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Unguja kisiwani  Zanzibar.Nape ameeleza kuwa taarifa rasmi ya yaliyohusu kikao hicho atayaweka wazi mapema kesho asubuhi.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link