Home » » Rais Kikwete aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Mjini Unguja

Rais Kikwete aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Mjini Unguja

Written By CCMdijitali on Tuesday, January 13, 2015 | January 13, 2015

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai leo alipofika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja akihudhuria Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa(katikati) Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mjumbe wa Kamti Kuu ya CCM Taifa Dk.Mohammed Gharib Bilali wakati alipowasili Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo katika Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
 Makam Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Haji Mkema mara alipowasili Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo alipohudhuria katika Kikao cha kawaida cha siku moja cha Kamati Kuu ya CCM Taifa (wa pili kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo walipohudhuria katika Kikao cha kawaida cha siku moja cha Kamati Kuu ya CCM Taifa.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wazee wa Chama cha Mapinduzi alipofika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo akihudhuria Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.










[Picha na Ikulu.]
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link