Katibu Mkuu wa CCM akizungumza na watoto wadogo wanaopata elimu ya awali kwenye skuli ya Donge Mtambile.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Kaskazini B kwenye ukumbi wa mikutano wa tawi la CCM Donge Kipange ambapo aliwapongeza wana CCM wa mkoa wa Kaskazini kwa kuwa na idadi kubwa ya wanachama wanaolipa ada ya uanachama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mzee Ali Ameir aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Donge,Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) mara baada ya kumaliza kikao cha Halmashauri kuu ya Wilaya ya Kaskazini B.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi mfuko wa saruji iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Donge kwa Mwalimu mkuu wa Skuli ya Donge Mtambile Bakari Ahmed Hussein, wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Done Sadifa Juma Hamisi(kushoto) na Mwenezi wa wilaya ya Kaskazini B Ndugu Haji Machano Haji (kulia)
Wakina mama wa kikundi cha ujasiriamalicha Donge Mtambile wakionyesha namna ya ukataji sabuni walizozitengeneza wenyewe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia bidhaa zinazotengenezwa kwa mkono na kikundi cha ushirika wa akina mama cha Donge Mtambile.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia na Mwenyekiti Kamati ya Skuli ya Sekondari Mahonda Ndugu Salum Ghalib Salum ambaye ni mwanachama wa chama cha CUF.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ukumbi wa kufanyia mitihani kwenye skuli ya sekondari Mahonda pamoja na Mbunge wa Jimbo la Donge Sadifa Juma Hamisi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na baadhi ya wananchi mara baada yakumaliza kuswali Ijumaa katika msikiti wa Mahonda wilaya ya Kaskazini B,Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pesa taslim shilingi laki nne kwa mama Sitti Mohamed wa kikundi cha Riziki yetu kutoka Kazole wilaya ya Kaskazini B zilizotolewa kwa vikundi 12 na Mama Asha , mke wa Balozi Seif Idd
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na wa mama wa kimakonde mara baada ya kuhutubia wakazi wa Tawi la CCM Mwembe Majogoo sehemu ambayo inasemekana wana mapinduzi walitokea .
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakionja mapishi ya wanafunzi wa chuo cha Kaskazini Unguja .
Wahamasishaji wakihamasisha kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa Maskani ya CCM Kizota, Mahonda wilaya ya Kaskazini B,Zanzibar.
Wananchi wa Wilaya ya Kaskazini B wakiwa makini kusikia hotuba mbali mbali kutoka kwa viongozi wao.
Mbunge wa Jimbo la Donge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa Sadifa Juma Hamisi akihutubia wakazi wa Kaskazini B na kuwaambia kuwa ametekeleza ahadi kwa asilimia kubwa na kuwataka vijana kuacha kuingia kwenye makundi ya watu watakaowatumia kisiasa.
Mke wa Balozi Seif Idd, Mama Asha akisalimia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mahonda ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mama Asha alitumia nafasi hiyo kwa kuwaambia vijana kabala hawajawa washabiki wa viongozi fulani kuna umuhimu watafute historia za viongozi hao.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Balozi Ali Karume akihutubia wakazi wa Kaskazini B kwenye viwanja vya Maskani ya CCM Kizota na kuwaambia Katiba mpya iliyopendekezwa ni nzuri sana kwa Wazanzibar lakini pia alisisitiza ni vyema Katiba hiyo iendane na Katiba ya Zanzibar hivyo kuna umuhimu wa kubadili Katiba ya Zanzibar.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa wilaya ya Kaskazini B kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya maskani ya CCM Kizota.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd akihutubia wakazi wa Mahonda ambapo aliwataka wana CCM Zanzibar kutokubali kurudishwa nyuma.
Mamia ya watu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Maskani ya CCM Kizota
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mahonda na kuwaambia CCM inatekeleza ilani yake vizuri na wataendelea kuisimamia Serikali katika kutimiza ahadi za mwaka 2010.
Viongozi wakisoma dua baada ya kumaliza mkutano salama.