Sherehe hiyo ilishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho kimesimamia mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo. Rais Kikwete pia ndiye mdhamini mkuu wa Mkataba huo.
Wengine walioshuhudia tukio hilo muhimu ni Rais wa Uganda, Mheshimiwa Jenerali Yoweri Kaguta Museveni; Rais Uhuru Muigai Kenyatta wa Kenya; Naibu wa Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa, Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mheshimiwa John Samwel Malecela ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo na Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Abdulrahman Kinana ambaye alikuwa mwezeshaji wa mazungumzo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akikaribisha viongozi na wajumbe katika mkutano huo
Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mheshimiwa John Samwel Malecela ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo akisoma muhtasari wa mazungumzo hayo
Sehemu ya ukumbi wa mkutano huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza utiaji wa saini wa Mhe. Salva Kiir Mayardit Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mheshimiwa Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakionesha hati baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pongezi kwa Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda akiongea
Dkt. Riek Machar akiongea
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiongea
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kulia) na Bw. Bw. Deng Alor Kuol wakifurahia wakati Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (wa pili kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini
Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Kikwete na Bw. Dkt Kuol wakipiga makofi wakati Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny wakipeana mikono kwa furaha baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini.
Naibu Rais wa Afrika ya Kusini Mhe Cyril Ramaphosa akiongea na kupongeza hatua iliyofikiwa
Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
Wajumbe wa kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO)
Sehemu ya wajumbe wa kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO)
Kila mtu alisimama kumshangilia Rais Kikwete
Wajumbe wa kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD)
Furaha kwa kila mtu
Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Abdulrahman Kinana ambaye alikuwa mwezeshaji wa mazungumzo akisoma dondoo za makubaliano
Meza kuu katika picha ya pamoja na kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG)
Picha ya pamoja na kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO)
Picha na Sekretareti ya mazungumzo hayo
Rais Kikwete na Mzee Malecela wakipongezana baada ya kufanikisha mazungumzo na hatimaye makubaliano ya viongozi wa SPLM