Wananchi wa Tanga
mjini wakimpa mkono wa kumuga Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara
baada ya kumaliza mkutano wake wa kuwashukuru Watanzania kwa kuichagua CCM na
kuwashukuru kwa imani yao kwa kutambua chama kinaweza kuongoza.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia
wananchi alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
uwanja wa Tagamano,mkoani Tanga,wa kuwashukuru wananchi walioichagua CCM kwenye
uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 2014 nchi nzima ambapo mkoa
wa Tanga umekuwa wa pili kwa kushinda kwa asilimia 97.Mzee Yusuf akiwasalimu wakazi wa Tanga mjini ambapo anatazamiwa kutumbiza jioni ya leo kwenye uwanja wa Mkwakwani ikiwa kama ahadi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyoitoa wakati wa ziara yake ya mkoa wa Tanga mwishoni mwa mwaka 2014.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa mkoa wa Tanga kwenye uwanja wa Tangamano ambapo alitoa salaam za mwaka huuambapo alisema CCM mwaka huu itaweka mkazo kwenye maadili ya Viongozi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa mkoa wa Tanga kwenye uwanja wa Tangamano ambapo alitoa salaam za mwaka huu ambapo alisema CCM mwaka huu itaweka mkazo kwenye maadili ya Viongozi.
Wananchi wakishangilia jambo
Wakazi wa mji wa Tanga wakiwa wamejitokeza kwa wingi jioni ya leo katika uwanja wa Tangamano,kwenye mkutano wa hadhara,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alizungumza nao kuwashukuru kwa kufanya vyema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni nchini Kote
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo mbele ya
maelfu ya wakazi wa mji wa Tanga,katika uwanja wa Tangamano jioni ya leo,baada
ya aliyewahi Kugombea Ubunge Tanga Mjini kwa tiketi ya chama cha CHADEMA mnamo
mwaka 2010,Kassim Omar Mbarak almaarufu Makubel,alipotangaza rasmi kuhamia
chama cha CCM,baada ya kuvutiwa na hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
alipozungumza na wakazi wa Mji wa Tanga kuwashukuru kwa kufanya vyema katika
uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni nchini Kote.