Diwani wa Kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega Vumi Magoti
akielezea kero za umeme katika kata yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto), viongozi na wananchi
(hawapo pichani).
Home »
» WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI
Written By CCMdijitali on Tuesday, January 6, 2015 | January 06, 2015
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco)
Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora
na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega kabla ya
kuanza ziara katika wilaya hiyo ili kujionea utekelezaji wa miradi ya umeme
vijijini pamoja na kuzungumza na wananchi.
Mkazi wa kijiji cha Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani
Simiyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza maswali mbele ya
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na wananchi
(hawapo pichani) mara Waziri alipofanya mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho
ili kusikiliza kero zao.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
akisisitiza jambo kwenye mkutano na wananchi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani
Busega.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia)
akitoa maelekezo kwa Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma (
wa mwisho kushoto) ya kuitaka Tanesco kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme
vijijini.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
akisisitiza jambo katika mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Bushigwamala
wilayani Busega (hawapo pichani).
Sehemu wananchi wa kata ya Kalemala wilayani
Busega waliojitokeza kwenye mkutano na Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo wakifuatilia kwa makini hotuba yake.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia)
akitoa maelekezo kwa mtaalamu kutoka kampuni ya Symbion iliyopewa kazi ya
kujenga miundombinu ya umeme katika kijiji cha Nyamikoma kilichopo wilayani
Busega Bw. Steve Thomson (kushoto).
Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma,
akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
na wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega (hawapo pichani).
Mkazi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega ambaye jina
lake halikupatikana mara moja akitoa hoja yake mbele ya Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto waliosimama mbele)
mara Waziri alipofanya ziara katika kijiji hicho na kusikiliza kero za
wananchi.