Pembeni kushoto ni mtapta wao Bibi Liu Hualian.
Dr. Liu Yaping kiongozi wa Madaktari wa Kichina wanaotoa huduma za Afya Hospitali za Zanzibar kati kati akiwa sambamba na Mtapta wao Bibi Liu Hualian wakiagana na Balozi Seif mara baada ya mazungumzo yao wakiomba kurudi nyumbani kwa mapumziko ya mwaka Mpya.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibart Balozi Seif AAli Iddi aagana na Madaktari Bingwa wa Kichina wanaotoa huduma za afya katika Hospitali mbali mbali hapa Zanzibar.
Madaktari hao wanatarajiwa kuondoka Zanzibar mwezi ujao kurudi nyumbani kwa kipindi cha mwezi mmoja wa mapumziko kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya wa Kichina unaoingia mwezi Febuari ya kila mwaka.
Madaktari hao ambao tayari wameshatoa huduma za afya Zanzibar kwa karibu mwaka mmoja na nusu sasa wanatarajiwa kurejea Zanzibar kuendelea na kazi hiyo mwezi wa machi mwaka huu wa 2015.