MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya ENGLAND MANCHESTER CITY imeambulia kichapo cha mabao mawili kwa bila kutoka wa ARSENAL katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa ETIHAD.
Mabao ya ARSENAL yamefungwa na SANTI CAZORLA kwa mkwaju wa penati na bao la pili likafungwa na OLIVIER GIROUD.
Katika mchezo mwingine West Ham United imeibuka na ushindi wa mabao MATATU kwa BILA dhidi ya Hull City.
Mabao ya West Ham United yamefungwa na Andy Carroll, Morgan Amalfitano na Stewart Downing
Msimamo wa EPL unaonyesha CHELSEA inaongoza ikiwa na ALAMA 52, Manchester City ipo katika nafasi ya pili na ALAMA 47, SOUTHAMPTON ya tatu na ALAMA 42, MANCHESTER UNITED nafasi ya NNE na ALAMA 40, ARSENAL inashika nafasi ya tano na ALAMA 39.
Santi Cazorla opens Arsenal's account with a penalty