Muumini wa Dini ya Kikiristo, Heema Said akitoa neno la shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete 9aliyevaa koti kushoto) alipokabidhi ambulance hiyo. Ridhiwani alisema kuwa yeye hivi sasa ni mbunge wa vyama vyote jimbo humo hivyo ambulance aliyoitoa itoe huduma kwa wakazi wote wa jimbo hilo bila kubagua watu kutokana na itikadi zao. Pia aliuasa uongozi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wanatunza vizuri gari hilo.
Dok Rutaihwa akimkabidhi ufunguo wa gari hilo Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Chalinze, Dk.Victor baada ambulance hiyo kukabidhiwa na Mbunge Ridhiwani.
Dk. Victor akitoa shukurani kwa Mbunge Ridhiwani kwa msaada huo wa ambulance
Wakifurahia kwa pamoja kupata usafiri huo muhimu kwa wagonjwa
Mbunge Ridhiwani Kikwete na Dk. Rutaihwa wakiangalia ndani ya ambulance hiyo
Wakiwa na furaha baada ya kuangalia samani zilizomo ndani ya ambulance hiyo
Ridhiwani pamoja na viongozi wa dini ya kiislamu wakiliombea dua gari hilo. Kutoka kulia ni Alhaji Sheikh Hussein Fuko na Alhajj Khamis Magula
Ridhiwani (katikati) na Mbuunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Chalinze akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk. Rutaihwa.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk.Mastidia Rutaihwa akitoa shukurani kwa Ridhiwani kwa msaada wa Ambulance na kuahidi kuitunza
Ridhiwani akipongezwa na wananchi kwa kuwapatia ambulance
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hafsa Kazinja akicheza muziki na mmoja wa wazee wa Chalinze alipotumbuiza katika mkutano huo
Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria makabidhiano ya ambulance katika viwanja vya miembe saba mjini Chalinze leo
Mbunge wa Jimbo la Mtera, Dodoma, Lusinde ambaye alikuwa safarini akitokea Dodoma kwenda Dar kwenye vikao vya Kamati za Bunge, aliamua kushiriki kwenye mkutano huo ambapo alimsifia Mbunge Ridhiwani kwa kipindi kifupi alichoaguliwa kuwa mbunge miezi sita iliyopita kutekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ikiwemo ambulance hiyo, ujenzi wa visima katika vijiji mbalimbali na ujenzi wa barabara pamoja na zahanati
Lusinde akikumbatiana kwa furaha na Ridhiwani baada ya mkutano huo kumalizika.