Naibu waziri wa Viwanda na Biashara JANET MBENE
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara JANET MBENE amevishauri viwanda vya vileo kutumia mazao yanayozalishwa nchini ili kuwawezesha wakulima kuwa na soko la uhakika la mazo yao.
Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda cha bia cha Serengeti cha mjini MOSHI mkoani KILIMANJARO, MBENE amesema malighafi kama shayiri, mtama na mahindi yanazalishwa kwa wingi hapa nchini na hivyo hakuna sababu ya viwanda kuagiza mazao hayo nje.
Naye Meneja wa kiwanda hicho, GIDEON KABUTHI amesema kiwanda chake kinakabiliwa na changamoto za kukatika kwa umeme mara kwa mara, jambo ambalo linaathiri shughuli za uzalishaji kiwandani hapo.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, JANET MBENE, amevitaka viwanda vinavyozalisha vyakula nchini kuzingatia usalama na ubora wa vyakula kwa kutumia vipimo sahihi vinavyobaini uhakika wa chakula kwa walaji.