Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Dkt. Asha-Rose Migiro akimtunuku shahada ya uzamili ya usimamizi wa miradi mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda katika mahafali ya 27 ya chuo hicho yaliyofanyika mjini DODOMA. Kushoto anayeshuhudia ni Makamu mkuu wa chuo hicho
Profesa Tolly Mbwete.
Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akitoka kupokea shahada ya uzamili ya usimamizi wa miradi. Akiongea baada ya hapo Mama Pinda ametoa wito kwa kinamama wa Tanzania na Afrika kwa jumla kujiendeleza kielimu ili kukomboa mataifa yako kutoka katika dimbwi la umaskini
Kikundi cha wake wa viongozi kutoka Dar es salaam kikimpongeza mlezi wao Mama Tunu Pinda kwa kutunukiwa shahada ya uzamili ya usamamizi miradi ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika mahafali ya 27 iliyofanyika Mjini Dodoma. Toka kushoto ni Mama Mashiba, Mama Lukuvi na Mama Malima .