Meneja Ufundi wa Kiwanda cha Magurudumu cha General Tyre cha jijini Arusha, Elias Pallangyo,akimuonyesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene , sehemu ya kiwanda hicho ambayo ipo katika ukarabati tayari kwa ajili ya uzalishaji wa Magurudumu mapema mwaka huu. Kiwanda hicho kitafufuliwa baada ya kufungwa tangu mwaka 2009.
Meneja Masoko wa Kiwanda cha A to Z cha jijini Arusha,Binnesh Harrier, akimuonyesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ,Janeth Mbene, namna fulana zinavyozalishwa kiwandani hapo juzi. Kiwanda hicho kinazalisha vyandarua, fulana zikiwemo bidhaa nyingine muhimu ambazo usafirishwa katika nchi zaidi ya 25 duniani.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha A to Z cha jijini Arusha kujionea hali ya uzalishaji .