Rais Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo maalum ya Vision 2025 Big Results Now kwa Rais Mstaafu wa Botswana Mheshimiwa Dkt. Festus Mogae aliyeongoza jopo maalum la kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi tuzo maalum ya Vision 2025 Big Result Now kwa Dkt. Sipho Moyo, Mkurugenzi Mtendaji wa ONE wa Kanda ya Afrika aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa jopo la kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa. Rais Kikwete aliwakabidhi tuzo hizo huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi Tuzo Maalum ya Vision 2025 Big Results Now kwa Bwana James Adams, Makamu wa Rais Mstaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa miongoni mwa wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) huko Ikulu tarehe 16.01.2015.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Jopo la Kutathmini Programu ya Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN Independent Review Panel). Kulia kwa Mheshimiwa Rais Kikwete ni Rais Mstaafu wa Botswana Dkt. Festus Mogae akifuatiwa na Bwana James Adams (Makamu wa Rais Mstaafu wa Benki ya Dunia), aliyesimama wa kwanza kushoto ni Bibi Linah Mohohlo (Gavana wa Benki Kuu ya Botswana) na wa kwanza kulia ni Dkt. Sipho Moyo (Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Afrika, ONE. Waliosimama mstari wa nyuma (kulia kwenda kushoto) Dkt. Nkosana Moyo (Mwanzilishi wa Mandela Institute for Development Studies) akifuatiwa na Lord Peter Mandelson (Mwenyekiti, Global Counsel ‘Uingereza’), anayefuata ni Bwana Knut Kjaer, (Mwenyekiti, Trident Asset Management, ‘Norway’) PICHA NA JOHN LUKUWI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Ijumaa, Januari 16, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo na wajumbe wa Kamati Maalum Inayojitegemea Iliyofanya Tathmini ya Utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam
Rais Kikwete amewashukuru wajumbe wa Kamati Maalum Inayojitegemea iliyofanya tathmini ya utekelezaji wa Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Kikwete amewashukuru kwa kazi nzuri wajumbe hao saba wa Kamati hiyo ya BRN Independent Review Panel ikiongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana, Mheshimiwa Festus Mogae.
Wajumbe
Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni pamoja na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. James Adams, aliyekuwa Waziri katika Serikali ya Bwana Tony Blair ya Uingereza Lord Mandelson, Gavana wa Benki Kuu ya Botswana Bi. Linah Mohohlo, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya ONE Bi. Sipho Moyo.
Wengine ni Bwana Knut Kjaer kutoka Norway na Bwana Nkosana Moyo.
Wajumbe hao wamekutana kwa siku mbili kuanzisha Alhamisi, Januari 15, 2015 mjini Dar es Salaam ambako wametathmini mwaka wa kwanza wa utendaji wa BRN baada ya kuwa wamepokea maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Presidential Delivery Bureau (PDB), mawaziri sita ambao wanaongoza sekta ambazo ziko katika BRN kwa sasa na timu maalum ya Kampuni ya PWC ambayo ilifanya ukaguzi matokeo ya utendaji ya mwaka wa kwanza wa BRN.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
16 Januari,2015