Home » » WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, PROFESA SOSPETER MUHONGO AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO ASISITIZA SIKU ZA KUUNGANISHA UMEME KUPUNGUA

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, PROFESA SOSPETER MUHONGO AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO ASISITIZA SIKU ZA KUUNGANISHA UMEME KUPUNGUA

Written By CCMdijitali on Sunday, January 18, 2015 | January 18, 2015

"Kwa kipindi kirefu, serikali imekuwa inatoa fedha nyingi kuisaidia Tanesco kutekeleza miradi katika maeneo ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme hivyo Bodi hii ionyeshe jinsi mtakavyolibadilisha Shirika hili ili hii misaada kutoka serikalini ipungue na ifike mahala Shirika hili lijitegemee," alisema Profesa Muhongo. 
"Bodi simamieni maombi ya kufungiwa umeme ambayo sasa yanaelezwa kushughulikiwa ndani ya siku 30, hii lazima ibadilike, watanzania lazima wapewe umeme ndani ya wiki, zaidi ya hapo haikubaliki. 
"EWURA waelezwe kuhusu suala hili ili kuona namna ya kupunguza hizi siku sababu wao wanahusika katika suala la upangaji wa siku husika," alisisitiza Profesa Muhongo. 


  Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwapongeza Wajumbe wa Bodi mpya ya TANESCO mara baada ya kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam na kutoa vipaumbele vya utekelezaji wa majukumu. Wanaoshuhudia ni viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Naibu Waziri, Stephen Masele (kushoto kwa Waziri) na Kaimu Katibu Mkuu, Eng. Ngosi Mwihava (wa nne kulia).
  Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo mara baada ya kuzindua Bodi mpya ya TANESCO katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini  Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa tatu kutoka kushoto), Kaimu Katibu Mkuu, Eng.Ngosi Mwihava (wa nne kutoka  kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Eng. Felchesmi Mramba (wa nne kulia). Wengine katika picha ni Wajumbe wa Bodi hiyo, Eng. Juma Mkobya,(wa tatu kulia), Bw. Felix G. Kibodya  (wa pili kulia), Bibi. Kissa Vivian Kilindu (wa kwanza kulia), pamoja na watendaji mbalimbali wa TANESCO (waliokaa mstari wa nyuma).
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kutoka kushoto),Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa tatu kutoka kushoto), Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng.Ngosi Mwihava (wa nne kutoka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Eng. Felchesmi Mramba (wa pili kulia),wakimsikiliza mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO (haonekani pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni mmoja wa wajumbe wa Bodi  hiyo, Eng. Juma Mkobya.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Dkt. Mighanda J. Manyahi (aliyesimama) akizungumza mara baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Waziri, Profesa Muhongo (kulia) na Mjumbe wa Bodi hiyo, Dkt. Haji H. Semboja (kushoto). Wajumbe wa Bodi ya TANESCO wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Mighanda J. Manyahi (wa sita kutoka kushoto)wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng.Ngosi Mwihava (wa tano kulia) mara baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.Wajumbe wengine wa Bodi hiyo (kutoka kushoto) ni Dkt. Nyamajeje C. Weggoro, Eng. Boniface C. Muhegi, Dkt. Mutesigwa I. Maingu, Bw. Shaaban S. Kayungilo, na Dkt. Haji H.Semboja. Wajumbe wengine (kutoka kulia) ni Bibi. Kissa Vivian Kilindu, Bw.Felix G. Kibodya na Eng. Juma F. Mkobya.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link