Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizindua mradi wa maji uliojengwa kwa msaada wa shirika la Oxyfarm katika kijiji cha Mvumi mission,jimbo la Mtera wilayani Chamwino.Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde ( Kibajaji )
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wakazi wa kijiji cha Mvumi mission,jimbo la Mtera mapema leo mara baada ya kuzindua mradi wa maji uliojengwa kwa msaada wa shirika la Oxyfarm
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo la Mtera,katika kijiji cha Mvumi Mission ,wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na viongozi wengine wa wilaya na mkoa wa Dodoma wakikagua mradi wa ujenzi wa madarasa shule ya Msingi Suli yaliyogharamiwa na shirika la Neigbourhood kutoka Korea ya Kusini,kwa kiasi cha shilingi bilioni tatu,ujenzi huo pia unahusisha vyumba vya walimu pamoja zahanati ya kijiji cha Suli.
Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde a.k.a Kibajaji akimwagilia maji mti alioupanda katika shule ya sekondari Fufu,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Kinana alikagua bweni la wasichana na kupanda miti katika suala zima la kulinda mazingira.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutanno huo wa hadhara.
Mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde (Kibajaji ) akiwahutubia wananchi wa Fufu,jimbo la Mtera wilayani Chamwino .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa Fufu,jimbo la Mtera wilayani Chamwino .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia baadhi ya wakazi wa kijiji cha Manzase kata ya Fufu,,jimbo la Mtera wiyani Chamwino mkoani Dodoma,leo jioni katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Manzase.
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Manzase Kata ya Fufu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia mapema leo jioni katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Manzase.