Home » » WATALII KUANZA KUFURIKA KIGOMA

WATALII KUANZA KUFURIKA KIGOMA

Written By CCMdijitali on Wednesday, April 8, 2015 | April 08, 2015

Treni mpya ya kisasa (Deluxe Train)

By Katuma Masamba, Kigoma (UHURU)

BAADA ya kuanzishwa kwa treni mpya ya kisasa (Deluxe Train), Mkoa wa Kigoma unatarajia kupokea idadi kubwa ya watalii, watakaoenda kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo.
Imeelezwa kuwa idadi ya watalii wanaotembelea imekuwa ndogo kuliko vituo vilivyoko. Kwa kiasi kikubwa hali hiyo imedaiwa kuwa inachangiwa na usafiri wa treni ya awali, ambao hauna uhakika na huchukua muda mrefu zaidi.

Kauli hiyo imetolewa na Mhifadhi Mkuu wa Makumbusho ya Dk David Livingstone na Henry Morton Stanley, Kassim Govola wakati akizungumza na gazeti hili kuhusu hali ya utalii na ujio wa treni hiyo mpya, iliyoanza safari zake mkoani humo, treni ambayo inatajwa kusimama katika vituo 14 pekee.

Alisema mkoa huo kuna maeneo mengi ya utalii na alitaja baadhi yake kuwa ni Hifadhi ya Sokwe ya Gombe ambayo ni ya kipekee katika Afrika Mashariki, njia ya miembe ya watumwa inayokwenda hadi Bagamoyo, Hifadhi Mahale na maeneo mengine.

Govola alisema kwa kawaida imekuwa ni vigumu kwa watalii wa kutoka nje ya nchi na wa ndani, kusafiri kwa kutumia muda mrefu kwenda kutembelea vituo vya utalii vilivyoko mkoani.

“Kwanza nitoe shukrani zangu kwa serikali kuanzisha treni hii, kwa sababu sasa idadi ya watalii itaongezeka maana wengi walikuwa wanashindwa kuja kwa sabnabu huku ni mbali sana na treni ile ya zamani inachukua muda mrefu,” alisema Govola.

Share this article :

+ comments + 1 comments

April 8, 2015 at 8:13 AM

Hongera Jakaya Kikwete.... kazi umefanaya kiongozi wetu !!

Post a Comment
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link