Home » » Kauli ya Mwalimu Nyerere kuhusu Edward Lowassa kwenye NEC Dodoma mwaka 1995

Kauli ya Mwalimu Nyerere kuhusu Edward Lowassa kwenye NEC Dodoma mwaka 1995

Written By CCMdijitali on Monday, August 3, 2015 | August 03, 2015

Dk Slaa katumia miaka 10 kumsema Lowasa,leo anaambiwa apande jukwaani akamsafishe dhidi ya matapishi yake.
Msekwa umenena.



Mwalimu Nyerere katika kitabu chake, Nyufa, cha mwaka 1995, alisema: “Sasa Tanzania inanuka rushwa… tunataka kiongozi anayejua hivyo, ambaye atasema rushwa kwangu mwiko, mwaminifu kabisa kabisa, hawezi kugusa rushwa na… watoa rushwa watamjua hivyo. Lakini hatutaki aishie hapo tu, maana haitoshi wewe mwenyewe uwe mwaminifu… Unaweza ukawa wewe mwaminifu kabisa kabisa, lakini una shinikizo la ndugu zako, jamaa zako na marafiki zako.

“Kwa hiyo si inatosha wewe kuwa mwaminifu tu, lakini uwe na uwezo wa kuwaambia jamaa zako kwa kauli ambayo wataiheshimu na hawatarudia tena. Unawaambia jamaa na rafiki zako kwa dhati kabisa… Ikulu ni mahali patakatifu, mimi sikuchaguliwa na wananchi wa Tanzania kuja kupageuza pango la walanguzi na hakuna serikali yoyote duniani inayoongozwa bila miiko”.

Zipo taarifa zinazoeleza kwamba fedha nyingi zimetumika katika kufanya maandalizi ya mkutano wa Arusha uliosababisha mafuriko ya watu. Aidha, ndugu Lowassa mara kadhaa amekiri kwamba marafiki zake ndio wanaomchangia kufanikisha safari yake ya matumaini.

Hivyo fedha nyingi anazochangia kwenye harambee kwenye misikiti na makanisani nyingine anatoa yeye na nyingine anachangiwa na hawa marafiki zake ambao wengi wao ni wafanya biashara matajiri na wengi wao ni wale waliotajwa kwenye kashfa za ufisadi na tuhuma mbalimbali.

Hawa marafiki zake Lowassa wamesaidia sana kumjua Lowassa ni nani, kwani wahenga walisema, “Nionyeshe marafiki zako na mimi nitakuambia wewe ni nani au wewe una tabia gani”.

Hawa marafiki zake na Lowassa wanaweza kuwasababisha Watanzania wamtilie shaka Lowassa kama anaweza kuwa safi na kustahili kupewa dhamana ya kuongoza nchi.

Kauli ya Mwalimu Nyerere kuhusu mmoja wa wagombea urais kwenye NEC Dodoma mwaka 1995, “Hapa hatuchagui mtu maarufu, tunachagua mtu safi na huyu si safi”.

“Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe nae chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Hapa mnasema ni tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni, Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike”.

“Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba si kweli. Lakini Kaisari bado akamwacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na sisi hapa mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine wasafi ambao hawana tuhuma.

“Kama mtamteua huyu mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu nimwombee kura. Hapana kabisa . Huyu najua si msafi na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa mgombea wetu”.

Mwaka 1995, kundi la Vijana lilimtaka Lowassa ateuliwe kugombea urais wa Tanzania. Hata hivyo, ilitolewa kauli kuwa Lowassa alikuwa na tuhuma za rushwa, kujilimbikizia mali na kupungukiwa na maadili, kinyume na katiba ya CCM na kanuni za chama hicho.

Kamati Kuu ilipopeleka mapendekezo ya kutompendekeza kugombea urais, Lowassa alitetewa kwa makelele, kihuni, bila kufuata taratibu za kikao cha NEC Dodoma. Kundi moja lilikuwa limejiandaa kumpitisha kwa hoja ya nguvu na si kwa nguvu ya hoja.

Waliyatetea maelezo ya Kamati Kuu, lakini waliyakataa yale ya nyongeza aliyoyatoa Mwenyekiti Ali Hassan Mwinyi (Rais wa wakati huo) ambaye alielezea tuhuma hizo zilizokuwa zinamkabili Lowassa. Hivyo, naomba kusisitiza kwamba Lowassa hakuwa chaguo la CCM katika uchaguzi wa mwaka 1995.

Katika kikao hicho cha Kamati Kuu, Mwalimu Nyerere aliamua kusaidia kikao kwa kutoa maelezo ya nyongeza. Aliwauliza wajumbe wa NEC maswali, kwamba wao ni wahuni au ni viongozi wa CCM? Ikiwa wao ni viongozi wa CCM, je, hivyo ndivyo wanavyopaswa kumtafuta mgombea wa urais, kwa makelele?

Kama Watanzania wangewaona walivyokuwa wanafanya katika kikao hicho, je, wangeamini kuwa wao ni viongozi kweli? (Wajumbe walibaki kimya). Kisha Mwalimu aliendelea kusisitiza maelezo aliyoyatoa Mwenyekiti Ali Hassan Mwinyi akisema: “Mwinyi amemstahi sana Lowassa”.

Hakuwaambia wajumbe wa NEC baadhi ya tuhuma mbaya kabisa kuhusu Lowassa.

Ikiwa NEC inachoombwa ni kuchagua kati ya wenye tuhuma za rushwa kuchaguliwa kwa nafasi ya urais, na wale wasioitaka, basi huu ni wakati muafaka kwao kuipeleka hoja hiyo mbele ya Watanzania waiamue kwa kuwa ndani ya NEC hakuna mwenye uwezo wa kumfukuza mwenzie, wote ni wajumbe sawa kwa mujibu wa katiba ya CCM”.

Hatimaye kikao cha NEC kiliondoa jina la Lowassa, kikawateua Benjamin William Mkapa, Cleopa David Msuya na Jakaya Mrisho Kikwete kuwa wagombea. Majina yao yaliwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu ambao ndio uliopaswa kumchagua miongoni mwao kuwa mgombea urais wa CCM.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link