Vijana wa Mjini wakiserebuka wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Uchaguzi ya Jimbo la Kikwajuni ilyofanyika Miembeni Jitini Mjini Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya CCM Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi Seif akimnadi mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kikwajuni kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mhandisi Hamad Masauni Yussuf.
Balozi Seif akimnadi mgombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Jimbo la Kikwajuni Nd. Nassor Salim Ali Jazeera.
Balozi Seif akiwakabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Ndugu Mbarouk Abdulla Hanga wa kwanza kutoka kushoto anayewania Uduwani Wadi ya Rahaleo na Nd. Ibrahim Khamis Fataki Ngasa Udiwani Wadi ya Kikwajuni kwa tiketi ya CCM.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Uchaguzi ya CCM Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba wananchi wa Jimbo la Kikwajuni wana kila sababu ya kuwaunga mkono Viongozi waliothibitishwa na CCM kugombea nafasi za Uongozi wa Jimbo hilo ili liendelee kuongozwa na chama hicho.
Balozi Seif alisema Viongozi wa Jimbo la Kikwajuni na lile lililokuwa Rahaleo walifanya kazi kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita katika kusimamia Maendeleo ya Wananchi wa Majimbo hayo walipojizatiti kukabiliana na matatizo ya Kijamii.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizindua Rasmi Kampeni ya Uchaguzi ya Jimbo la Kikwajuni kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mkutano uliofanyika katika uwanja wa Miembeni Jiti kubwa Mjini Zanzibar.
Alisema changamoto ya upatikanaji wa huduma za maji safi na salama ilipunguwa kwa kiasi kikubwa ndani ya Majimbo hayo kutokana na umahiri mkubwa ulioonyeshwa na Viongozi hao katika kuwatumikia wananchi wao ndani ya kipindi hicho cha miaka mitano.
Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi aliwaasa Wanachama wanaowania nafasi mbali mbali za Uongozi wahakikishe wachunga lugha zao wakati wa kuomba kura kwa wananchi.
Alisema Chama cha Mapinduzi {CCM } hivi sasa kina kundi moja tu baada ya kumalizika kwa mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama hicho ambalo ndilo linalotarajiwa kuleta ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu kwa ngazi zote ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.
Mapema Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mjini Bibi Fatma Shomari alisema licha ya baadhi ya viongozi wa upinzani kujaribu kutumia lugha za ulaghai katika kuomba kura lakini Jimbo la Kikwajuni litaendelea kuongozwa na Chama cha Mapinduzi.
Bibi Fatma alisema kinachotarajiwa na Wazanzibari na Watanzania waliowengi ni kuona sera sera zinazotekelezeka ambazo si nyengine bali ni za Chama cha Mapinduzi.
Katika Mkutano huo wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Jimbo la Kikwajuni Balozi Seif alipata fursa ya kuwanadi wagombea wote wa Chama cha Mapinduzi kwa Wananchi hao wa Jimbo la Kikwajuni.
Wagombea hao ni Mhandisi Hamad Masauni Yussuf nafasi ya Ubunge, Nassor Salim Ali Jazeera Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Nd. Ibrahim Khamis Fataki Ngasa Udiwani Wadi ya Kikwajuni na Nd. Mbarouk Abdulla Ngasa Diwani Wadi ya Rahaleo.
Wakiomba kupigiwa kura katika uchaguzi Mkuu ujao wagombea hao wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Kiwajuni wameahidi kufanya kazi za kwa ushirikiano ili kusimamia maendeleo ya Wananchi wa Jimbo la Kiwajuni.