Home » » Majambazi wanne wauliwa na Polisi miongoni mwao watatu ni raia wa Kenya

Majambazi wanne wauliwa na Polisi miongoni mwao watatu ni raia wa Kenya

Written By CCMdijitali on Friday, September 18, 2015 | September 18, 2015

 Picha mbalimbali za vifaa walivyokutwa navyo majambazi hao watatu Raia wa kenya na mmoja mtanzania
 



Waandishi wa habari wakiangalia gari walilokuwa wakilitumia majambazi hao lilivyopigwa risasi


WATU watatu wanaosadikiwa ni majambazi ambao ni raia wa Kenya pamoja na Mtanzania mmoja wameuwa katika majibizano na polisi eneo la Chekereni mpakani mwa wilaya ya Arumeru na Jiji la Arusha.

Aidha majambazi hayo yamekufa kwasababu ya ushirikiano kati ya jambazi mmoja aitwaye Sixtus Ngowi (51) ambaye alikamatwa awali na kutoa ushirikiano kwa polisi kuwa anashirikiana na wenzake hao watatu raia wa Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini hapa, 
Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema polsi walipokea taarifa za kiintelijensia Agosti 19 /2015 juu ya kuwepo kwa kundi la majambazi wanaotoka nchini Kenya na kuja Mkoani Arusha kwa lengo la kufanya uporaji kwakushirikiana na majambazi wenzao hapa nchini.

Alisema kutokana na taarifa hizo polsi walizifuatilia na kufanikiwa
kumkamata Ngowi mkazi wa Ngulelo Jijini Arusha na 
baada ya mahojiano kwa kina ,Ngowi alikiri kuwa yeye ni  miongoni mwa majambazi ambaye anashirikiana na majambazi hao kutoka nchini Kenya na kufanya matukio
mbalimbali nchini Tanzania.

Marehemu Ngowi alikiri kuhusika na tukio la uporaji
 kwenye kampuni ya Security Group 4 akiwa na wenzake na kuiba dola za Kimarekani 2,000,000 Jijini Dar es Salaama mwaka 2005 na baadaye kufikishwa mahakamani.

Lakini pia mwaka 2002 Ngowi pamoja na wenzake 
alihusika katika tukio la uvamizi kwenye benki ya NBC Tawi la Moshi Mkoani Kilimanjaro mbali na matukio hayo mwaka 2014 Machi aliwahi kushtakiwa Nchini Kenya katika mahakama ya Kilimani Law Court Jijini Nairobi lakini baadaye
aliachiwa huru.

Ngowi kabla ya kwenda na polisi kufanikisha mtego wa 
majambazi wenzake wa Kenya aliwataja kwa jina moja moja 
baadhi ya majambazi aliokuwa
akishirikiana nao kuwa ni Kamau, Bon, Mike, Kim, Katiwa na wengine ambao alisema hawajui kwa majina lakini wanatokea nchini Kenya huku hapa nchini alimtaja mshirika wake aitwaye Richard mkazi wa Dar es Salaam.

Pia Ngowi aliendelea kukiri kushirikiana na wenzake 
kuhusika kwenye matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha katika Jiji la Arusha yaliyotokea juni 23/2015 na Agosti 17/2015 ambapo walengwa walikuwa ni wafanyabiashara wakubwa wanaojihusiha na biashara ya madini ya Tanzanite na Hoteli za Kitalii.

Miongoni mwa wafanyabiashara hao ni pamoja na Mathias Manga ambaye ni Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) ambaye alijeruhiwa kwenye ubavu wa kulia kwa risasi katika jaribio la kupora fedha na madini na alipokuwa kwenye muendelezo wa mahojiano jambazi
huyo aliahidi kushirikiana na polisi kupatikana kwa wenzake.

Na siku ya juzi Septemba 17/2015 wakiwa kwenye mpango wa kuvamia mojawapo ya duka ya kubadilisha fedha liitwalo sanya la Jijini hapa ,Ngowi alikubali kuongozana na askari kwaajili ya kufanikisha kupatikana kwa wenzake lakini kabla ya kuwakamata walipofika eneo la Chekereni majambazi hao raia wa Kenya walishtuka kuwa walioongozana
na mwenzao ni askari polsi na wao kuanxa kupiga risasi na kufanikiwa kumjeruhi Ngowi aliyekuwa katika gari nyingine iliyokuwa na polisi hao  na alikufa akipelekwa hospitalini.

Baada ya tukio hilo polisi waliamua kujibu mapigo na kufanikiwa
kuwauwa watu watatu ambao ni Simon Kariuki, Bonifas Mbulu na Thadeo Njuguna huku wengine wakitoroka ambao walikuw akatika gari namba T981AVK aina ya Noah.

Katika eneo la tukio ilibainika kuwa majambazi hao watatu kila mmoja alikutwa na bastola pamoja na risasi , magegi matatu meusi ambapo baada ya kuyafungua walikuta bunduki aina ya AK 47 mbili zenye namba 83LG 3953 56-1 na nyingine yenye maandishi ya kirusi na SMG namba 56-128038394 ,bastola tatu zenye namba CZ 75 Compact Luger- 9mm namba a.269206, CZ 85 B LUGER 9mm namba 051967 na Chines Pistol namba
967741, magazine nne za ziada tupu za smg, risasi 85 za 
SMG /Ak 47 na risasi 28 za bastola.

Vitu vingine walivyokutwa navyo ni Radio Call mbili aina ya Kenwod na Charger moja zilizokuwa hewani na mawimbi ya polisi Arusha, Bullet Proof moja, vifaa vya kusafisha Bunduki (Gunslick), tochi kubwa tatu,
mbili kati a hizo ni aina ya DP na moja ni Panasonic, mashuka ya
kimasai matatu ,mifuko mitau ya kubebea fedha ,gloves za vitambaa ,kofia mbili aina ya boshori ambazo katika tukio la kumvamia mfanyabiashara aitwaye Manga zilitambulia pia kulikutwa na koti moja lenye muenekano wa sare za kijeshi.

Pia marehemu hao watatu raia wa Kenya walikutwa na vitambulisho vitatu vya nchini Kenya veyen majina ya Simon Kariuki, Bonifas Bulu na Thadeo Njuguna na kitambulisho kimoja cha UN-ICTR chenye jina la Chacha marwa , leseni ya udereva iliyotolewa Kenya yenye jina la Thadeo Njuguna, Kadi ya Benki ya Equity, Master Card yenye jina la Somon Githinji pamoja na kadi ya benki ya Cooperative baki yenye jina la Thadeo Njuguna simu tano aina ya Nokia , Tecno na Samsung.

Polisi wanaendelea na upelelezi juu ya tukio hilo pamoja na kuwatafuta watuhumiwa wengine ambao walitoroka katika tukio na kubaini mtandao wa majambazi hao kwani kwa mujibu wa polisi kuwa kwataarifa alizozitoa Ngowi kabla ya kufa zinadai kuwa majambazi hao wa Kenya walitumwa na
wenzao ambao wanatumikia vifungo kutokana na wizi wa beni za NBC na NMB Moshi Mkoani Kilimanjaro na kuhukumiwa vifungo waliwatuma kutafuta fedha ili familia zao ziweze kuendelea kuishi wakiwa  wanaendelea kutumikia vifungo .

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwaajili ya utambuzi kutoka kwa ndugu na jamaa zao wa karibu.

Mwisho.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link