MUIMBAJI Maarufu wa nyimbo za Injili jijini Arusha Tuponile Komba ambaye ni Askari wa Kikosi cha zima moto na uokoaji amezindua Albam yake ijulikanayo kwa jina '' kesho yako inakuja ''yenye nyimbo nane iliyofanyika katika Kanisa la EAGT Elerai lililopo Sakina Jijini Arusha .
Akitumbuiza nyimbo zake ambazo zilikuwa za kufurahisha mbele ya maelfu ya watu waliokusanyika Kanisani hapo ambapo pia aliambatana na waimbaji mbalimbali kutoka jijini Dar es Salaam pamoja na wengine kutoka jijini hapa huku Mgeni Rasmi akiwa ni mfanyabiashara maarufu wa madini Jijini Arusha John Mafie.
Akizungumza na Gazeti hili aliseama kuwa anamshukuru Mungu kwa uzinduzi huo kwani ni albamu ya pili ya kwanza ni yesu akisema ndiyo hakuna awezaye kupinga yenye nyimbo nane kuwa kukamilisha hii ametumia miezi saba mbali na kwamba amekuwa na changamoto za muda kutokana na kazi zake lakini amefanikiwa.
Aidha alisema kuwa mbali na kwamba ni mfanyakazi wa Serikali amekuwa akitenga muda ili kufanya kazi ya Mungu kwani malengo yake ni kuhakikisha anatimiza lengo lake la kuhubiri Injili kwa njia ya nyimbo.
Alisema lengo la kuzindua Albamu hiyo ni ili kupata kiasi cha shilingi milioni Therathini kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa mahospitalini,kuwasaidia yatima pamoja na kupeleka Injili vijijini kwani waimbaji wengi wanaishia mijini kutokana na ukosefu wa kipato hivyo yeye amejizatiti kuhakikisha anawafikia walengwa.
Kwa upande wake Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo Marko Haule alisema kuwa smefurahishwa na muibaji huyo kwa jinsi alivyojikita kusaidia jamii na kiwango alichokihitaji kinathihirisha kuwa anakusudi ,kwani waimbaji wengi wamekuwa wakitaja fedha nyingi na wengine kwa maslahi yao binafsi.
Alisema kuwa waimbaji wanapaswa kuiga mfano bora wa Tuponile huku wakionyesha nidhamu wakati wanaimba ,mavazi yao yawe mazuri huku wakitambua kuwa wao ni kioo katika jamii na wakristo wanajifunza kupitia wao.
Mwisho