Hatimaye Job Yustino Ndugai CCM amechaguliwa kuwa Spika
wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kuchaguliwa kwa kura 254 sawa na asilimia 70% ya kura zilizopigwa akifuatiwa na mgombea wa
CHADEMA Goodluck Ole Medeye ambaye
amepata kura 109.
Hata hivyo wagombea hao ambao walikuwa 7 kati ya 8
wameweza kutoa shukrani na pongezi kwa Ndugai
wakisema anastahili na ndio maana akachaguliwa na
kumtaka aongoze vyema bunge hilo.
Job Ndugai ameibuka mshindi wa kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata kura 254 sawa na asilimia 70 ya kura zote ambapo jumla ya kura zilizopigwa ni 365
Matokeo ya kura za Spika.
A: Job Ndugai (CCM)- 254
B: Goodluck Ole Medeye (CHADEMA) - 109
C: Hashimu Rungwe (CHAUMA)- 0
D: Peter Sarungi (AFP) -0
E: Dkt Godfrey Malisa (CCK)- 0
F: Richard Lymo (T.L.P) -0
G: Robert Kisinini (DP) -0
Kura zilizoharibika ni 2