Home » » DED wa Arusha ahimiza uwekezaji vitega uchumi

DED wa Arusha ahimiza uwekezaji vitega uchumi

Written By CCMdijitali on Tuesday, February 16, 2016 | February 16, 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha, Juma Idd

Imeandikwa na Veronica Mheta, Arusha /Habari Leo

WANASIASA na viongozi wengine mkoani Arusha wameshauriwa kuhamasisha wawezekaji wa ndani kuwekeza katika maeneo yaliyobomolewa nyumba na Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa ajili ya ujenzi wa vitega uchumi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Juma Idd wakati alipokuwa akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani.


Alisema wanasiasa wana nafasi kubwa ya kuhamasisha wawekezaji katika maeneo hayo yakiwemo eneo la Kaloleni na Themi jijini hapa.


Alisema katika maeneo hayo kulikuwa na nyumba zilizobomolewa kupisha ujenzi wa vitega uchumi mbalimbali.


Alisisitiza kwamba maeneo hayo hayatatolewa kinyemela.


Aidha Mkurugenzi huyo aliwataka madiwani kwa kushirikiana na viongozi wa kata zao kusimamia kikamilifu na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu unaosababishwa na uchafu wa mazingira.


Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro alisema halmashauri hiyo imewaelekeza wataalamu wake kuja na miradi michache ambayo inatekelezeka kwa wakati. Alisema hivi sasa hawatakuwa na miradi mingi ambayo mwisho wa mwaka haimaliziki.


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link