Pongezi hizo amezitoa mara baada ya kupokea taarifa za mafanikio hayo kutoka kwa muuguzi,mkunga mshauri wa kituo hicho Elizabeth Mshana baada ya mjumbe huyo na msafara wake wa viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo wilaya ya Arusha kwaajili ya kuwafariji wagonjwa na kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
Akitoa maelezo hayo Mshana alisema tangu kuanza kwa utolewaji wa huduma hizo katika kituo hicho miaka miwili iliyopita hakuna motto yeyote aliyegundulika na virusi vya Ukimwi kutokana na kuambukizwa na mama yake wakati akiwa tumboni wala wakati wa kunyonyeshwa.
Alisema wapo akina mama wengi wajawazito waliogundulika mapema katika hatua za mwanzo za ujauzito kuwa na virusi vya Ukimwi ambapo walipatiwa maelekezo kuhusu kuwakinga watoto wao na kwamba wote walifika kwa wakati na mapema hakuna aliyeweza kumuambukiza mtoto.
Alisema kwa takwimu za hivi karibuni kuna jumla ya akina mama wajawazito wapatao 25 waliogundulika kuwa na maambukizi ya Ukimwi ambapo kati yao watoto15 waliokingwa waliweza kufanikiwa kuzaliwa salama huku wengine wakisubiriwa wajifungue ili kujua iwapo watoto wao wako salama au laa.
Alisema idadi hiyo ya watoto waliofanikiwa kukingwa za kuzaliwa salama kwa sasa wapo katika hatua ya kunyonyesha ambapo wanasubiriwa tena muda huo upite ili wapimwe ili kuonekana kama wapo salama au laa.
Kufuatia taarifa hiyo Mamuya alitoa pongezi zake na kusema wanachokifanya wahudumu hao ni kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli kupitia kauli mbiu yake yake ya Hapa Kazi Tuu na kuwataka kuendelea kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu hiyo.
Aidha aliwataka watumishi hao kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu hiyo kwa akina mama wote wanaofika katika kituo hicho ili kuwakinga watoto na watu wa jamii yao dhidi ya maradhi mbalimbali yakiwemo yale ya mlipuko kama kipindupindu.
Akizungumza na wanawake waliofika na watoto wao kupata huduma mbalimbali aliwataka kuendelea kufuata taratibu zote za afya ya uzazi ikiwemo kuwahi hospitalini mara tu wanapojihisi kuwa wajawazito ili kuondokana na madhara wanayoweza kuyapata kwa kuchelewa.
Alisema vifo vingi vya wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka 5 vimekuwa vikitokea kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kizembe na zinazoweza kuepukika ikiwemo kuchelewa katika vituo vya afya.
Pia aliwataka wakina mama hao kuhakikisha wanawaelimisha waume zao juu ya kupima afya wao na wake zao wakati wa ujauzito kama hatua ya kumwandaa mtoto salama badala ya kuendelea kuwaacha bila elimu hiyo wanayoipata wao katika vituo hivyo.
Pia aliahidi kufikisha kilio cha kituo hicho cha afya ikiwemo uhaba wa madawa,vyumba vya kulaza wagonjwa,ukosefu wa vifaa vya upasuaji pamoja na majengo mengine yakiwemo ya utawala ambayo inasababisha kero mbalimbali kwao na kwa wagonjwa wanaowahudumia.
Katika maadhimisho hayo mjumbe huyo pamoja na viongozi na wanachama aliofuatana nao walitoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa wagonjwa na wazazi ikiwemo sabuni za kufulia,kuogea,mafuta ya kujipaka na vingine vingi ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti kuzunguka kituo hicho.
Kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa CCM kinatarajiwa kuwa mnamo Februari 6 mwaka huu huko mkoani Singida katika uwanja wa Namfua ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mwenyekiti wa CCM taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwisho.
MJUMBE wa Baraza Kuu la UWT Taifa Bi Halima Mamuya akimpongeza Bi Amina Yusuph kwa kujaliwa mtoto salama katika Kituo cha Afya cha Kata ya Daraja ii, Jijini Arusha
Baadhi ya Viongozi wa Chama Kata na UWT akiwafariji wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Kata ya Daraja ii, Jijini Arusha
MJUMBE wa Baraza Kuu la UWT Taifa Bi Halima Mamuya akimpongeza Bi Amina Yusuph kwa kujaliwa mtoto salama katika Kituo cha Afya cha Kata ya Daraja ii, Jijini Arusha
Bi Jazla Mohamed akitabasamu kwa furaha kwa kujaliwa mtoto salama katika Kituo cha Afya cha Kata ya Daraja ii, Jijini Arusha
MJUMBE wa Baraza Kuu la UWT Taifa Bi Halima Mamuya akiwa amempakata mtoto aliyezaliwa salama katika Kituo cha Afya cha Kata ya Daraja ii, Jijini Arusha
MJUMBE wa Baraza Kuu la UWT Taifa Bi Halima Mamuya akisalimiana na Muuguzi Bi Tabitha Peter na kuimpongeza Bi Josepha T Silayo aliyekwenda kiliniki katika Kituo cha Afya cha Kata ya Daraja ii, Jijini Arusha
Bi Tabitha Peter Muuguzi katika Kituo cha Afya cha Daraja ii
MJUMBE wa Baraza Kuu la UWT Taifa Bi Halima Mamuya akisaini kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Chama ya Kata ya Daraja ii, Jijini Arusha
MJUMBE wa Baraza Kuu la UWT Taifa Bi Halima Mamuya akivishwa vazi alilopewa zawadi na Uongozi wa UWT Kata ya Daraja ii ,katika Ofisis ya Chama Kata ya Daraja ii, Jijini Arusha
MJUMBE wa Baraza Kuu la UWT Taifa Bi Halima Mamuya akipewa taarifa ya Chama na jumuiya ya UWT kutoka kwa Katibu wa CCM Kata ya Daraja ii Ndg Kifumba, katika Ofisi ya CCM Kata ya Daraja ii, Jijini Arusha
Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Bano akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi za CCM Kata ya Daraja II.
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua.