Diwani wa Chadema Mh Msofe amejikuta chini ya ulinzi kwa kukiuka taratibu na kanuni za uchaguzi kwa kufanya kampeni siku ya kupiga kura za marudio leo katika Mtaa wa Sanare ,Kata ya Daraja II.
Kijana wa Chadema naye ajikuta mikononi mwa Sheria ,baada ya kutumia bendera ya chama chake kutaka kipigiwe kura,katika eneo la kupigia kura.
Madiwani wa Chadema Kata za Themi na Olmoti wakodiwa kuongeza nguvu Uchguzi wa Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Sanare leo.
Diwani wa Chadema Mh Msofe,akiondolewa kwenye eneo linalofanya uchaguzi leo,katika Mtaa wa Sanare,Kata ya Daraja II
Aliyesimama kulia akiwa ameweka mikono mfukoni ni mwanachama wa Chadema aliyekuwa anatumia bendera ya chama hicho kwenye eneo la uchguzi leo
Wananchi wenye hasira kali,wakihakikisha Diwani Msofe anaondolewa kwenye Mtaa huo, kwa kukutwa akifanya Kampeni kwenye Mtaa wa Sanare leo.Uchaguzi huu unarudiwa baada ya matokeo ya awali ,wagombea wote kutoka suluhu kwa idadi ya kura sawa CCM 381 ,Chadema381
Madiwani wa Kata ya Themi (aliyevaa jeans) na Olmoti (mbele ya mama mwenye blausi ya mistari) wakiwa katika eneo la uchaguzi leo, katika Mtaa wa Sanare. Baada ya Wakaazi kuwalalamikia kuwa huo uchaguzi hauwahusu kwani siyo wakaazi wa eneo husika ,ilibidi waondoke.
Wakazi wa Mtaa wa Sanare ,wakitimiza haki yao ya Kikatiba ya kumchagua kiongozi wanayemtaka,katika foleni.
Diwani wa Chadema Mh Msofe,akiongea na baadhi ya Viongozi wa CCM kwenye eneo linalofanya uchaguzi leo katika Mtaa wa Sanare,Kata ya Daraja II
Wakazi wa Mtaa wa Sanare ,wakitimiza haki yao ya Kikatiba ya kumchagua kiongozi wanayemtaka,katika foleni.
Diwani wa Chadema Mh Msofe (aliyevaa kofia),akiongea na Katibu wa CCM Kata ya Daraja II Ndg Mkombozi Kifumba (kushoto mwenye nguo nykundu na mistari meupe) kwenye eneo linalofanya uchaguzi leo katika Mtaa wa Sanare,Kata ya Daraja II
Wakazi wa Mtaa wa Sanare ,wakitimiza haki yao ya Kikatiba ya kumchagua kiongozi wanayemtaka,katika foleni.
Gari ya Polisi ikiwa imemchukua kijana aliyekuwa anatumia nembo ya Chama chake kwenye eneo la Uchaguzi leo,akipelekwa kituo cha Polisi.
Kiongozi wa Polisi akiondoa watu waliokuwa wamejazana kwenye kituo cha kupigia kura,wakitakiwa wawe mbali na kituo hicho mara baada ya kupiga kura.
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha,Ndg jasper Kishumbua