Katibu Mwenezi CCM Wilaya ya Arusha,katika ziara ya Kujenga Chama Kata ya Themi katika picha na Waasisi wa Chama Cha Mapinduzi 30 Aprili 2016
Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Themi,Bi Wandera Mikidadi - Katibu wa Uchumi na Fedha Kata akichukua kumbukumbu , katika kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halamashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama inayofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika Kata zote 25 ndani ya Jiji la Arusha 30 Aprili 2016.
Kaimu Katibu wa Kata ya Themi Bi Mary Kanora akimkaribisha Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua, katika kikao cha Semina ya Kujenga Chama kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halamashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa, 30 Aprili 2016.
Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Themi,Bi Wandera Mikidadi - Katibu wa Uchumi na Fedha Kata akichukua kumbukumbu , katika kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halamashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama inayofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika Kata zote 25 ndani ya Jiji la Arusha 30 Aprili 2016.
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua
Press Release:-
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua katika Semina hiyo aliwataka Viongozi wote wa ngazi zote kuhakikisha wanafanya vikao kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama Cha Mapinduzi.
Aliwakumbusha kuzingatia na kuelewa Malengo na Madhumuni ya CCM,ili chama kiweze kuwa Imara.
Pia aliwasisitizia kuheshimu Masharti ya Uanachama kwa mujibu wa Katiba na kuhakikisha kila Mwanachama anatekeleza wajibu wake wa kulipa ada ya Uanachama kama inavyoelekezwa kwenye Katiba ya Chama Cha Mapinduzi 1977, toleo la 2007 ,Ibara ya 12 (a),(b) na (c)
Aliwataka Viongozi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kumuunga mkono Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John P. Magufuli,katika jitihada anazofanya za kutumbua majipu, kwani ni katika kurekebisha na kurejesha Nidhamu, Uadilifu na Uwajibikaji Serekalini, kama ilivyo katika Ilani ya CCM, ili Watanzania wote waweze kufaidika na matunda ya Nchi yao.
Tunapozungumzia amani na utulivu ni pamoja na kuhakikisha kwamba walio chini wapo vizuri.
Alibainisha kuwa kama hawatakuwa vizuri ,hapatakuwepo na Amani na Utulivu .
Aliwasihi Viongozi wa ngazi zote na Wanachama kuwapuuza wanaosema kuwa Mh Rais amechukua mambo ya Ukawa, kwani hata hiyo Ilani ya Ukawa ninaidownload mpaka leo sijafanikiwa, kwani yote anayoyafanya yamo katika Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi 2015 (Ibara ya 185 (c)Maadili na Miiko ya Uongozi,(d)Mapambano dhidi ya Rushwa na 186 Kukua kwa tofauti kubwa ya kimapato katika Jamii) ,aliyoinadi kwa Watanzania na kuikubali na kukipa Chama Cha Mapinduzi ridha ya kushika dola.
Aliwataka Viongozi katika ngazi zote,kutimiza Jukumu la CCM ,kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015, Ibara ya 189.