Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akiongea na viongozi waliofika katika Semina iliyofanyika katika Ofisi za CCM Kata ya Ngarenaro 30 Aprili 2016.
Ikiwa muendelezo wa ziara aliyoianza 18 Aprli 2016 mpaka 22 Mei 2015.
Kaimu Mwenyekiti wa Kikao hicho na Katibu wa Kata Bi Krisanta Mwenyemvua akimkaribisha mgeni rasmi katika semina ya Kazi ya Kujenga Chama inayofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akiwataka Viongozi wa ngazi wa ngazi zote kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kupata taarifa za kila baada ya miezi mitatu,kama inavyoelekezwa kwenye Ilani aliyoishika mkononi kwenye ziara ya Kujenga Chama Kata ya Ngarenaro30/04/2016
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Arusha Ndg Musa Mkanga akiwasalimia wajumbe wa Semina hiyo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Ngarenaro.
Katika picha ni Wajumbe wa Sekretarieti wa Kata ya Ngarenaro
Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Ngarenaro, katika kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halamashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama iliyofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika Kata hiyo 30 Aprili 2016.
Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Arusha Ndg Musa Mkanga akiwa meza kuu na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha,akifuatiwa na Kaimu Mwenyekiti wa Kikao hicho na Katibu wa Kata Bi Krisanta Mwenyemvua na Katibu wa Siasa na Uenezi Ndg Yussuf Sharif,wakisikiliza hoja za Wajumbe kwa makini.
Mmoja wa Viongozi waliokuwepo wakiupongeza Uongozi wa CCM Wilaya ya Arusha kwa kufanya ziara ilyokuja kuibua uhai wa Chama katika Kata hiyo.
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua